Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Kusaya amewataka wale wote waliojinufaisha na mali za vyama vya ushirika hapa Nchini kurudisha Mali zote walizochukua kinyume na utaratibu akionya kuwa kwa kushindwa kufanya hivyo serikali itawafuata na hizo mali watazirudisha kama ambavyo baadhi yao wameanza kufanya.
Aidha Kusaya ameongeza kuwa mipango ya kufanya mabadiliko ya Uongozi katika Chama cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) yako mbioni akisema kuwa mabadiliko hayo ni suala la wakati kwani mipango ya Serikali ni kuhakikisha Vyama vya Ushirika vinajiendesha kibiashara na kwa faida.
Katibu Mkuu Gerald Kusaya amesema hayo jana wakati Kamati ya Maalum ya iliyoundwa na Waziri Mkuu kufuatilia Mali za SHIRECU ilipokabidhi mali nane za SHIRECU zenye thamani ya Bilioni 3.3 ikiwemo viwanja na Ghara la kuifadhia mizigo liliko Kurasini pamoja na nyumba moja iliyoko Ilala Jijini Dar es Salaam.
Hati za Mali za Chama Cha Ushirika Mkoa wa Shinyanga SHIRECU ziliwasilishwa kwake na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Asangye Bangu ambaye alisema kamati yake tayari imewezeza kurejesha Mali nane ambazo zinajumuisha ardhi, mitambo na nyumba zilizo kuwa nje ya SHIRECU na sasa zimerejeshwa katika Chama hicho.
Bangu amesema kuwa kipindi cha mwaka 2000hadi 2005 baadhi ya viwanja ambavyo vilikuwa mali ya SHIRECU vilichukuliwa kwa njia za ujanja ujanja na baadhi ya Maafisa Ardhi wa Manispaa ya Shinyanga kwa kujimilikisha wenyewe na vingine kuviuza na wamiliki viwanja hivyo kwa kuwa walisha viendendeleza walitoa viwanja vingine vinye ukubwa na thamani sawa na viwanja walivyochukua ambavyo Sasa ni mali ya SHIRECU.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Zainab Telack alisema sasa SHIRECU inahitaji utaalam na utawala wa kuiwezesha kujiendesha kwa kuwa tayari ina mali nyingi akitaja Jengo la Ghorofa Tatu liloko Ilala na Ghala la liliko Kurasini Jijini Dare es Salaam ambalo pia lina sehemu yenye kiwanda cha kusindika Kahawa kama sehemu ya mali inayotosha kuendesha kibiashara Shirika hilo.
Aidha Telack ameongeza kuwa ni lazima SHIRECU ijiendeshe kutokana na mali zilizopo kwa kuwa sasa Shirika hilo halikopeshiki kutokana na kuwa na mzigo mkubwa wa madeni ambapo kwa sasa inadaiwa zaidi ya Bilioni 15 ukiachilia mbali madai ya watumishi.
Mali za Vyama vya Ushirika nchini zinarejeshwa kufuatia Agizo la Rais John Magufuli alilotoa Mwaka 2016 katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza kutaka wale wote waliochukua mali za Vyama vya Ushirika bila kufuata utaratibu kuzirejesha na baadae kuundwa Tume Maalum ya kufutilia mali hizo Tume iliyoundwa na Waziri Mkuu wa Tanzania kufuatia Agizo hilo.
No comments:
Post a Comment