Matokeo chanyA+ online




Tuesday, May 9, 2023

MHE. RAIS SAMIA SULUHU HASSAN AKUTANA NA KUZUNGUMZA NA WATANZANIA WANAOISHI NAMIBIA ‘DIASPORA’

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na baadhi ya Watoto wa Kitanzania wanaoishi nchini Namibia mara baada ya kuzungumza na Watanzania (Diaspora) katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek tarehe 08 Mei, 2023.

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Viongozi wa Watanzania (Diaspora) wanaoishi nchini Namibia mara baada ya kuzungumza nao katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Maafisa Ubalozi wa Tanzania nchini Namibia mara baada ya kuzungumza nao katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023.

 




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na baadhi ya Watoto wa Kitanzania wanaoishi nchini Namibia mara baada ya kuzungumza na Watanzania (Diaspora) katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek tarehe 08 Mei, 2023.

 





Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea zawadi Maalum kutoka kwa Viongozi wa Watanzania (Diaspora) wanaoishi nchini Namibia mara baada ya kuzungumza nao katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023, wakati Rais Samia alipokuwa akihudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Troika, na Nchi Zinazochangia Vikosi vya Jeshi vya Force International Brigade (FIB) uliofanyika jijini Windhoek nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Watanzania wanaoishi nchini Namibia (Diaspora) katika Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania Jijini Windhoek, mara baada ya kumalizika kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Troika, na Nchi Zinazochangia Vikosi vya Jeshi vya Force International Brigade (FIB) uliofanyika nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023.






Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uhusiano wa Kimtaifa wa Namibia Mhe. Netumbo Nandi – Ndaitwah, wakati Rais Samia alipokuwa akihudhuria Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Troika, na Nchi Zinazochangia Vikosi vya Jeshi vya Force International Brigade (FIB) uliofanyika jijini Windhoek nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023.


Monday, May 8, 2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Organ Troika, SADC Troika na Nchi zinazochangia Vikosi vya Jeshi katika Force Intervention Brigade (FIB)

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amesimama pamoja na Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakati Wimbo wa Taifa wa Namibia pamoja na ule wa SADC ukiimbwa kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Dharura wa Wakuu hao wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Organ Troika, SADC Troika na Nchi zinazochangia Vikosi vya Jeshi katika Force Intervention Brigade (FIB) Windhoek nchini Namibia tarehe 08 Mei, 2023.




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) Organ Troika, SADC Troika na Nchi zinazochangia Vikosi vya Jeshi katika Force Intervention Brigade (FIB)




NUKUU UTEKELEZAJI WA BAJETI YA WIZARA YA KILIMO 2022/2023











 

Saturday, May 6, 2023

RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN AKIONGOZA KIKAO CHA VIONGOZI MBALIMBALI WA SERIKALI KINACHOHUSU KUANZA KWA MCHAKATO WA KATIBA MPYA IKULU CHAMWINO MKOANI DODOMA







 

MAKAMU WA RAIS AKIWASILI BUJUMBURA BURUNDI MEI 06 2023


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Melchoir Ndadaye uliopo Bujumbura nchini Burundi na kupokelewa na Makamu wa Rais wa Burundi Mheshimiwa Prosper Banzombaza leo tarehe 06 Mei 2023. Makamu wa Rais anamwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa 11 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Wanachama wa Mpango wa Amani, Usalama na Ushirikiano kwaajili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Ukanda wa Maziwa Makuu unaofanyika Bujumbura nchini Burundi.


Kamishna wa Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. David Kafulila, akizungumza wakati akifunga rasmi kikaokazi kati ya Serikali na Wataalam kutoka Taasisi ya Benki ya Dunia inayojihusisha na utoaji wa mikopo na misaada ya kiufundi kwa Sekta Binafsi - International Finance Corporation (IFC), kilicholenga kupitia na kujadili miradi ya kimkakati ambayo Serikali inataka itekelezwe kwa njia ya ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP), kilichofanyika kwa siku 5 katika Ukumbi wa Hazina Ndogo, jijini Dar es Salaam.


Afisa Mwandamizi wa Uwekezaji na Huduma za Ushauri wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kutoka Taasisi ya Benki ya Dunia inayojihusisha na utoaji wa mikopo na misaada ya kiufundi kwa Sekta Binafsi - International Finance Corporation (IFC) Bi. Ramatou Magagi, akifundisha namna ya kuandaa miradi ya PPP, manunuzi Pamoja na namna ya kuandaa mikataba bora ya miradi ya ubia, kwa wataalam wa kitanzania kutoka TANESCO, TPA, DART, TRC, TANROADS, Wizara ya Madini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Vyuo vikuu vya Mzumbe na UDSM, TGDC na TPDC wakati wa kikaokazi kinachoendelea katika Ofisi Ndogo za Hazina Jijini Dar es Salaam, kikihusisha Serikali na Wataalam hao kutoka IFC.

Afisa Mwandamizi wa Uwekezaji Sekta ya Kimataifa ya Nishati kutoka Taasisi ya Benki ya Dunia inayojihusisha na utoaji wa mikopo na misaada ya kiufundi kwa Sekta Binafsi - International Finance Corporation (IFC) Bw. Stefan Rajaonarivo, akifundisha namna bora ya kuandaa miradi ya nishati kupitia njia ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) kwa wataalam wa kitanzania kutoka TANESCO, TPA, DART, TRC, TANROADS, Wizara ya Madini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Vyuo vikuu vya Mzumbe na UDSM, TGDC na TPDC wakati wa kikaokazi kinachoendelea katika Ofisi Ndogo za Hazina Jijini Dar es Salaam, kikihusisha Serikali na Wataalam hao kutoka IFC.
Mtaalam wa masuala ya Ubia kutoka Taasisi ya Benki ya Dunia inayojihusisha na utoaji mikopo na misaada ya kiufundi kwa Sekta Binafsi - International Finance Corporation (IFC) Bi. Caroline Eric, akifundisha namna ya kuandaa miradi bora na yenye sifa ya kuvutia mitaji kutoka sekta binafsi (PPP) kwa wataalam wa kitanzania kutoka TANESCO, TPA, DART, TRC, TANROADS, Wizara ya Madini, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Vyuo vikuu vya Mzumbe na UDSM, TGDC na TPDC wakati wa kikaokazi kinachoendelea katika Ofisi Ndogo za Hazina Jijini Dar es Salaam, kikihusisha Serikali na Wataalam kutoka IFC.

Wadau mbalimbali wa masuala ya Ubia kutoka taasisi mbalimbali za Serikali wakimsikiliza kwa umakini Kamishna wa Idara ya Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi, Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. David Kafulila akifunga rasmi kikaokazi kilichofanyika kwa siku 5 kati ya wataalam hao wa Serikali na Wataalam kutoka Taasisi ya Benki ya Dunia inayojihusisha na utoaji wa mikopo na misaada ya kiufundi kwa Sekta Binafsi - International Finance Corporation (IFC), katika Ofisi Ndogo za Hazina Jijini Dar es Salaam, kikihusisha Serikali na Wataalam hao kutoka IFC.


 

KATIKA KUDHIBITI KELELE NA MITETEMO HAYA HAPA MAELEKEZO YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ALIYOYATOA TAREHE 6 MEI 2023 KUONDOA UTATA WA MADHEHEBU YA DINI NA MAMLAKA YA UDHIBITI WA MAZINGIRA NEMC JUU YA JAMBO HILO