YALIYOJIRI JANUARI 14, 2018 KATIKA MAZUNGUMZO YA RAIS WA JMT, DKT. JOHN POMBE MAGUFULI NA RAIS WA RWANDA MH. PAUL KAGAME KATIKA ZIARA YAKE YA KIKAZI NCHINI TANZANIA.
#Rais wa Rwanda, Mh. Paul Kagame amewasili majira ya saa 4 asubuhi tarehe 14/1/2018 katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa JMT, Dkt. John Pombe Magufuli.
#Rais wa Rwanda, Mh. Paul Kagame yuko Tanzania kwa ziara ya kikazi ya siku moja ikiwa na lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Tanzania na Rwanda.
#Nimemuhakikishia kuwa Watanzania tutampa ushirikiano wa kutosha katika nafasi yake ya Uenyekiti wa Umoja wa Afrika - Rais Magufuli.
#Tumekubaliana kukuza biashara kati ya Rwanda na Tanzania kwa kutengeneza mazingira mazuri ya biashara - Rais Magufuli.
#Juhudi za kukuza biashara kati ya Rwanda na Tanzania zilishaanza, mwaka 2017 mizigo iliyofika katika Bandari ya Tanzania kutoka Rwanda ilifikia tani 950,000 - Rais Magufuli.
#Tumekubaliana na Rais Kagame kujenga reli ya kisasa kutoka Isaka, Tanzania hadi Kigali, Rwanda ili kuchochea maendeleo ya nchi hizi mbili - Rais Magufuli.
#Naomba Mawaziri wa Rwanda na Tanzania wanaohusika katika sekta ya miundombinu wakutane wiki hii ili kupanga juu ya ujenzi wa reli hiyo - Rais Magufuli.
#Tunataka ndani ya mwaka huu tuweke mawe ya msingi katika ujenzi wa reli hiyo ya kisasa ili ujenzi huo uanze rasmi - Rais Magufuli.
#Napenda kumpongeza Rais Kagame kwa hatua anazozichukua katika kuiletea maendeleo nchi ya Rwanda - Rais Magufuli.
#Nampongeza Mkuu wa Majeshi wa nchini Rwanda kwa kushirikiana na Mkuu wa Majeshi wa Tanzania katika kuimarisha usalama wa nchi zote mbili - Rais Magufuli.
#Wananchi wa Rwanda wanataka kufanya biashara na watanzania hivyo hii itapelekea kudumisha amani na umoja wetu na kuinua uchumi wa nchi zetu - Rais Kagame.
#Naahidi kuendelea kutembelea nchi ya Tanzania ili kupata ushauri kuhusu mambo mbalimbali yatakayotuletea maendeleo katika nchi zetu - Rais Kagame.
#Tatizo la ajira ni changamoto kwa Afrika nzima hivyo kila nchi inahitaji kukuza biashara na uwekezaji ili kuongeza upatikanaji wa ajira - Rais Kagame.
#Pia jukumu kubwa linabaki kwa vijana namna ambavyo wanaweza kutumia elimu na ujuzi walionao katika kujitafutia ajira - Rais Kagame.
IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI - MAELEZO.
No comments:
Post a Comment