Meli Mpya ya Kampuni ya Sea Star ikiwa imetia Nanga baada ya kuwasili katika Bandari ya Malindi Zanzibar.
-
Sehemu kubwa ya kuwekea Mizigo mbali mbali ndani ya Meli Mpya ya Sea
Star yenye uwezo wa kubeba mizigo Tani 1,400 na Abiria 1,500 ikiwepo
Bandariniu Malindi.
Sehemu za kukalia Watu Mashuhuri {VIP} zilizomo ndani ya Meli ya Sea Star.
Muonekano wa sehemu za nje za Abiri wa kawaida zilizopo juu kabisa ya Meli Mpya ya Abirina na Mizigo ya Kampuni ya Sea Star One.
Kepteni
wa Meli Mpya ya Sea Star Nassor Abubakar akimpatia maelezo Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kwenye Chumba cha
Mawasiliano alipofika kuikagua Meli hiyo.
Balozi
Seif na mwenyeji wake Mh. Salum Turky wakipumzika moja ya sehemu za VIP
baada ya kutembelea sehemu mbali mbali za Meli hiyo.
Mwakilishi
wa Kampuni ya Sea Star Mh. Salum Turky wa Tatu kutoka Kulia akisisitiza
azma ya Uongozi wa Kampuni hiyo kufuata Taratibu zote za usafiri wa
Baharini wakatiu choba chao kitakapoanza kutoa huduma ya usafiri.
Balozi
Seif akibadilishana mawazo na Uongozi mzima wa Sea Star juu kabisa ya
Meli ya Kampuni hiyo baada ya kumaliza ziara ya kuikagua sehemu mbali
mbali. Picha na – OMPR – ZNZ.
Meli
Mpya ya Kampuni ya Usafiri wa Baharini ya Sea Star yenye uwezo wa
kubeba Mizigo Tani 1,400 na Abiria 1,500 imewasili Bandarini Zanzibar
kwa ajili ya kuongeza huduma za Usafiri wa Baharini katika Mwambao wa
Bahari ya Afrika Mashariki.
Meli
hiyo iliyopewa jina la Sea Star 1 itafuatiwa na Boti nyengine Mbili za
Mwendo wa Kasi zinazotarajiwa kuingia Visiwani Zanzibar Mwezi Juni Mwaka
ujao wa 2019.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa na baadhi ya
Viongozi na Watendaji wa Mamlaka zinazosimmamia Usafiri wa Baharini
alipata nafasi ya kukagua sehemu mbali mbali za Meli hiyo iliyopo
Bandaini Malindi na kuridhika na Ubora wake.
Meli
hiyo yenye sehemu kubwa ya kubebea Mizigo, Vyumba vya Watu Mashuhuri {
VIP} pamoja na Abiria wa kawaida itaanza na safari za Zanzibar-Pemba –
Tanga, Zanzibar – Dar es salaa, Zanzibar – Mtwara na baadae kuendelea na
safari za mbali kwa kuanzia Visiwa vya Comoro.
Safari
ya Zanzibar - Dar es salaam huchukuwa muda unaokadiriwa wastan wa saa
Tatu wakati safari ya Zanzibar – Pemba itachukuwa wastani wa saa Nne na
Nusu.
Akitoa
Maelezo ya uwepo wa Meli hiyo Nchini Mwakilishi wa Kampuni ya Sea Star
Mh. Salum Turky alisema Uongozi wa Kampuni hiyo umejizatiti kutoa huduma
bora za Usafiri wa Baharini kwa Wananchi wote.
Mh.
Turky alisema miongoni mwa mambo yatakayozingatiwa na Uongozi huo
katika uendeshaji wa Biashara hiyo ni kuhusika katika kufuata taratibu
zote zilizoainishwa na Mamlaka ya Usafiri wa Baharini.
Alisema
Abiria wa kawaida atawajibika kulipia nauli shilingi 25,000/, Mtoto wa
kawaida atalipiwa Nusu Nauli na yule aliye na umri kati ya siku Moja
hadi Miaka Sita atachukuliwa bila ya malipo.
Mh.
Salum Turky alimueleza Balozi Seif kwamba Uongozi huo umeahidi
kuunganisha safari za Visiwa vya Comoro kufuatia ahadi aliyoitoa Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohamed Shein
katika kuimarisha uhusiano kati ya Zanzibar na Viosiwa hivyo.
Katika
kuimarisha huduma hizo za Usafiri wa Baharini Mwakilishi huyo wa Sea
Star aliiomba Serikali kuwapatia sehemu Maalum na ya uhakika kwa ajili
ya kuuzia Tiketi ili kuwaondoshea usumbufu Wananchi wanaohitaji huduma
hizo.
Naye
kwa upande wake Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mh. Hassan
Khamis Hafidh aliushauri Uongozi wa Sea Satar kwenda na ushindani wa
Kibiashara huku pia wakizingatia huduma nafuu kwa Wananchi.
Mh.
Hassan alisema Serikali imeamua kuweka milango wazi ya uwekezaji Nchini
katika azma ya kuona maeneo yote ya huduma za Umma yanawafikia vyema na
kwa wakati Wananchi walio wengi hasa wale wenye kipato cha chini.
Akitoa
shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
aliipongeza Kampuni hiyo ya Kizalendo kwa uwamuzi wake wa kuongeza
huduma za Usafiri wa Baharini Nchini.
Balozi
Seif alisema uamuzi wa Kampuni hiyo wa kuimarisha huduma za Usafiri
umekuja kwa wakati huku ukizingatia kwenda sambamba na mabadiliko ya
maisha ya Wananchi yanayowapa fursa ya kuingia katika mzunguuko wa
kibiashara unaohitaji zaidi huduma za usafiri.
Kampuni
ya Sea Star iliwahi kumiliki Boti Mbili ziendazo kwa kasi za Sea Star
One na Sea Star Two zilizotoa huduma za usafiri wa Baharini kati ya
Bandari ya Zanzibar na ile ya Dar es salaam kwa zaidi ya Miaka 13.
No comments:
Post a Comment