Kaimu
Mkurugenzi wa Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe (wa
pili kushoto) akimpa maelezo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme
(TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle (wa tatu kushoto) wakati
alipotembelea karakana ya Mt. Depot kukagua mashine ya kisasa ya
kukagulia magari iliyofungwa katika karakana hiyo. Kushoto ni Meneja wa
karakana hiyo Mhandisi Alex William.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle
(wa tatu kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa
Uzalishaji na Matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe (wa pili kushoto)
wakati alipotembelea karakana ya Mt. Depot kukagua mashine ya kisasa ya
kukagulia magari iliyofungwa katika karakana hiyo ili kurahisisha
utendaji kazi. Kushoto ni Meneja wa karakana hiyo Mhandisi Alex William.
Pichani,
gari linaonekana likiwa limenyanyuliwa juu na mashine ya kisasa (3D
Wheel Allignment) tayari kwa kuanza kukaguliwa, mashine hiyo ya kisasa
imefungwa katika karakana ya TEMESA Mt. Depot Keko Jijini Dar es Salaam.
Wakala wa Ufundi na Umeme TEMESA una mpango wa kufunga mashine nyingine
kama hizo katika karakana za mkoa wa Mwanza na Dodoma.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle
katikati akikagua maboksi maalumu ya kuhifadhia mtambo wa kuongozea taa
za magari (traffic light controller) katika karakana ya Mt. Depot kikosi
cha Umeme. Kushoto ni Kaimu meneja wa kikosi hicho Mhandisi Pongeza
Semakuwa na wa pili kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uzalishaji na
Matengenezo Mhandisi Sylvester Simfukwe.
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO - (TEMESA)
No comments:
Post a Comment