Mkuu
wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (rtd) Nicodemus Elias Mwangela amewataka
Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA) kukamilisha miradi ya ujenzi wanayo
pewa ndani ya muda wa makubaliano ya mikataba.
Brig.
Jen. (rtd) Mwangela ameyasema hayo jana wakati akishuhudia utiaji saini
wa mikataba miwili ya ujenzi wa Nyumba ya Mkuu wa Mkoa na ya Katibu ya
Katibu Tawala Mkoa kati ya TBA na Katibu Tawala Mkoa wa Songwe.
“TBA
mna sifa nzuri ya kujenga majengo ya serikali kwa kuzingatia ubora
unaotakiwa na kwa gharama nafuu lakini kuna wakati kunakuwa na kusita
katika kuwapa kazi kutokana na historia yenu ya kuchelewesha kukamilisha
miradi mnayopewa ya ujenzi”, ameeleza Brig. Jen. (rtd) Mwangela.
Ameongeza
kuwa TBA wamechelewesha ujenzi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na ujenzi wa
Hospitali ya Mji wa Tunduma hivyo ucheleweshaji huo usirudie katika
mikataba hiyo miwili waliyopewa kwani hatasita kuvunja mikataba hiyo
endapo wataonyesha ucheleweshaji.
Naye
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe David Z. Kafulila ameishukuru serikali ya
awamu ya Tano chini ya Rais John Pombe Magufuli kwa kuupatia Mkoa wa
Songwe kiasi cha shilingi bilioni 26.8 kwa ajili ya ujenzi wa miradi
mbalimbali mkoani hapa.
Kafulila
amesema serikali imekuwa ikitoa fedha za miradi mbalimbali lakini kasi
ya utoaji wa fedha na matumizi ya fedha hizo kwenye miradi husika
imekuwa haiendani na hivyo kusababisha kuchelewa kukamilika kwa miradi
hiyo.
Kwa
upande wake Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa Songwe Mhandisi Fidelis Cosmas
ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwa amini na kuwapa miradi hiyo
miwili yenye thamani ya shilingi bilioni moja na kuahidi kuikamilisha
kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.
Mhandisi
Cosmas amesema hapo awali walikuwa na changamoto kama vile ukosefu wa
maji, umeme na baadhi ya vifaa lakini wamesha zifanyia kazi changamoto
hizo hivyo watamaliza miradi hiyo Juni 30, 2019 kama walivyokubaliana
katika Mikataba.
Katibu
Tawala Mkoa wa Songwe David Z. Kafulila akisaini mikataba ya Ujenzi wa
nyumba za Mkuu wa Mkoa na ya Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, ambapo Wakala
wa Majengo (TBA) wamekubali kukamilisha ujenzi huo kwa muda wa miezi
mitano na kwa gharama ya shilingi bilioni moja.
Katibu
Tawala Mkoa wa Songwe David Z. Kafulila na Kaimu Meneja wa TBA Mkoa wa
Songwe Mhandisi Fidelis Cosmas wakisaini mkataba wa ujenzi wa nyumba za
Mkuu wa Mkoa na Katibu Tawala Mkoa, wa Kwanza Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Songwe Brig. Jen. (Rtd) Nicodemus Mwangela.
No comments:
Post a Comment