Mwanamitindo
na muigizaji maarufu Marekani aliyewahi kung’ara katika taji la Miss
Universe, Marisela De Montecristo aliwasili nchini hivi karibuni
ametembelea Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na kupokelewa na Mkuu wa
Idara ya Utalii katika Hifadhi hiyo.
Muda
mfupi baada ya kuwasili Mwanamitindo huyo aliyekuwa ameongozana na Mama
yake mazazi pamoja na anayetajwa kuwa mchumba wake ,alikabidhiwa zawadi
mbalimbali yakiwemo mavazi maalumu yanayotumiwa na Jamii ya Maasai.
Marisela
baada ya kutembelea mane mbalimbali ya Hifadhi hiyo wakiwemo wanyama
alieleza furaha yake huku akiahidi kuwa balozi wa vivutio vya utalii
atakavyotembelea hapa nchini .
Mrembo
huyo ambaye kwa sasa anaishi Los Angels amesema lengo la kuja nchini
kutembelea vivutio vya utalii ni pamoja na kuangalia fursa mpya
ipatikanayo katika sekta ya Utalii Duniani pamoja na kuvitangaza.
Mwanamitindi
huyo anaendelea na ziara yake hiyo ya kitalii katika Hifadhi ya
Ngorongoro ambako atashuhudia maajabu ya wanyama katika Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) na Bonde la ufa la Ngorongoro (Ngongoro
Creator).”
No comments:
Post a Comment