Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle
(wa pili kushoto aliyevaa suti) akipewa maelezo na wafanyakazi wa kivuko
cha MV. MKONGO mara baada ya kukagua kivuko hicho. Kivuko cha MV.
MKONGO kinatoa huduma katika mto Rufiji kati ya Mkongo na Utete wilayani
Rufiji mkoani Pwani na kina uwezo wa kubeba abiria 40 kwa wakati mmoja.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle
kulia akikagua mashine ya kupimia uwiano wa tairi za magari katika
karakana ya TEMESA mkoa wa Manyara wakati wa ziara yake mkoani humo.
Kushoto ni Meneja wa Temesa mkoani Manyara Mhandisi Margreth Julian.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Y. Maselle
(wa pili kushoto) akishuka kutoka kwenye kivuko cha MV. MALAGARASI mara
baada ya kumaliza kukagua utendaji kazi na hali ya usalama wa kivuko
hicho kinachotoa huduma katika mto Malagarasi kati ya Ilagala na Kajeje
mkoani Kigoma, kivuko hicho kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6
sawa na tani 50. Wa kwanza Kushoto ni Nahodha wa kivuko Kassimu
Mkitege.
Abiria
wakiingia katika kivuko cha MV. MALAGARASI tayari kuanza safari kutokea
upande wa Ilagala kuelekea upande wa Kajeje, kivuko cha MV MALAGARASI
kinatoa huduma katika mto Malagarasi kati ya Ilagala na Kajeje mkoani
Kigoma na kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 sawa na tani 50.
Kivuko
cha MV. MALAGARASI kikielea katika mto Malagarasi, kivuko hicho cha
tani 50 kina uwezo wa kubeba abiria 100 na magari 6 kwa wakati mmoja na
kinatoa huduma kati ya Ilagala na Kajeje mkoani Kigoma.
Nahodha
wa Kivuko cha MV. MALAGARASI Kassimu Mkitege kushoto akiwa na Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Mhandisi Japhet Maselle kulia
wakati alipokua akikagua hali ya usalama na utendaji kazi wa kivuko
hicho. Kivuko cha MV MALAGARASI kinatoa huduma katika mto Malagarasi
kati ya Ilagala na Kajeje mkoani Kigoma.
PICHA ZOTE NA ALFRED MGWENO - (TEMESA)
No comments:
Post a Comment