Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt.
Islam Seif Salum Mchenga kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu
(Deep Sea Fishing Authority –
DSFA).
Taarifa
iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi
wa Dkt. Mchenga umeanza tarehe 01 Desemba, 2018 na kwamba kabla ya uteuzi huo
alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi - Zanzibar.
Wakati huo huo,
Mhe. Rais Magufuli amemteua Dkt. Emmanuel Andrew Sweke kuwa Naibu Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA).
Uteuzi
wa Dkt. Sweke umeanza tarehe 01 Desemba, 2018 na kabla ya uteuzi huo alikuwa
Afisa Utafiti wa Uvuvi Mwandamizi na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa
Uvuvi Tanzania (Tanzania
Livestock Research Institute - TAFIRI) – Kigoma.
Katika hatua nyingine,
Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Sebastian W. Chenyambuga kuwa Mwenyekiti wa
Bodi ya Taasisi ya Utafiti wa Mifugo (TALIRI).
Uteuzi
wa Prof. Chenyambuga umeanza tarehe 26 Januari, 2019.
Halikadhalika,
Mhe. Rais Magufuli amemteua Prof. Justinian Rwezaula Ikingura kuwa Mwenyekiti
wa Bodi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (Geological
Survey of Tanzania - GST).
Uteuzi
wa Prof. Ikingura umeanza tarehe 18 Januari, 2019.
No comments:
Post a Comment