Serikali
iliwalipa stahili zote Watumishi wa Kiwanda cha nguo cha KILITEX
kilichopo mkoani Arusha baada ya kufungwa kutokana na tatizo la ukosefu
wa mtaji na malimbikizo ya madeni.
Hayo
yamebainishwa Bungeni Jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango
Dkt. Ashatu Kijaji, alipokua akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti
Maalaum Mhe. Catherine Magige, aliyeuliza ni lini Serikali itawalipa
wafanyakazi 545 wa KILITEX ambao bado wanadai pensheni baada ya kiwanda
hicho kufungwa ilihali mwajiri wao hakuwasilisha michango yao kwenye
Mfuko wa Kijamii wa PPF.
Dkt.
Kijaji alisema kuwa, kwa mujibu wa kumbukumbu na nyaraka za ufilisi,
taratibu za ufilisi zilikamilika na wafanyakazi hao walilipwa stahiki
zao kwa mujibu wa Sheria ya Makampuni namba 46 ya mwaka 1931.
“Baadhi
ya wafanyakazi walilipwa mafao ya kiinua mgongo kwa mkupuo na wengine
walirejeshewa michango yao kwa kadiri walivyochangia baada ya Mfilisi
kushindwa kulipa riba, adhabu na malimbikizo ya michango kwenye mfuko wa
Pensheni wa PPF”, alisema Dkt. Kijaji.
Alisema Kiwanda hicho kilisimamisha shughuli za uzalishaji mwaka 1994 na kuwekwa chini ya ufilisi na PSRC mwaka 1995.
Aidha
akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mlimba, Mhe. Suzan Kiwanga,
alietaka kufahamu ni lini wafanyakazi 11075 wa Shirila la Reli la
Tanzania na Zambia- TAZARA waliostaafishwa kwa lazima miaka 55 mwaka
2005, watalipwa mafao yao.
Alisema
Serikali imefuatilia madai hayo na takwimu sahihi ni wastaafu 271
walistaafishwa na madai yao yanashughulikiwa ili waweze kulipwa mafao
yao.
No comments:
Post a Comment