Naibu
waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega,akizungumza na baadhi ya
viongozi wa wilaya ya Singida kabla ya kuanza ziara ya uhamasishaji wa
kuogesha ng'ombe katika kijiji cha Mgori.
Bw.Rashid
Mandoa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Singida akitoa
taarifa kwa Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega.
Bw.Elia
Digha,Mwenyekiti wa halmashauri ya Singida akitoa ujumbe kwa Naibu
waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega (hayupo pichani)kuhusu
kuweka mikakati katika sekta ya mifugo nchini.
Naibu
waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega akikagua ng'ombe katika
kijiji cha Mgori kilichopo Singida vijijini alipokuwa ameenda kuzindua
zoezi la uhamasishaji wa kuogesha mifugo.
Baadhi
ya ng'ombe wakisubiri kuogeshwa dawa katika josho la Mgori katika
hamshauri ya wilaya ya Singida vijini ambapo Naibu waziri wa Mifugo na
Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega alizindua zoezi la uhamasishaji wa kuogesha
mifugo.
Naibu
waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega,akichanganya dawa za
kudhibiti magonjwa ya mifugo katika kijiji cha Mgori kwa ajili ya
kuhamasisha kuogesha ng'ombe katika majosho yalipo nchini ambapo
Serikali imeamua kutoa dawa bure kwa wafugaji.
Naibu
waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega akisaidiana na baadhi ya
wafugaji kuingiza mifugo katika josho lenye dawa ambazo zimetolewa bure
na Serikali zoezi hilo la uzinduzi katika mkoa wa Singida lilifanyika
katika kijiji cha Mgori kilichopo halmshauri ya wilaya ya Singida
vijijini.Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog
Na.Alex Sonna,Singida
Serikali
imeandaa mkakati wa kuboresha sekta ya mifugo pamoja na kudhibiti
magonjwa ya mifugo huku ikiwahimiza wafugaji kuzingatia matumizi ya
majosho yenye dawa.
Akizungumza
na wafugaji Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdalah Ulega wakati
wa zoezi la uhamasishaji wa uogeshaji wa ngo’mbe kanda ya kati mkoani
Singida, katika kijiji cha Mgori kilichopo halmshauri ya wilaya ya
Singida vijijini.
Katika
uhamasishaji huo waziri Ulega aliwataka wafugaji kufanya zoezi la
uogeshaji wa mifugo uliyoanzishwa uwe wenye tija na endelevu, kwa vile
hivi sasa hakuna sababu za kushindwa kuogesha mifugo yao katika majosho
yenye dawa ya kudhibiditi kupe.
Aidha
amesema kuwa kwa sasa serikali katika zoezi hili, imetoa dawa bure kwa
halmashauri zote nchini, na kukarabati majosho yote yaliyokuwa hayafanyi
kazi, ili wafungaji waweze kuogesha mifugo yao , kukinga ugonjwa hatari
unaoenezwa na kupe, ambao unaoongozwa katika vifo vya ng’ombe hapa
nchini.
"Mwanzo
shughuli hizo zilikuwa zikifanywa kwa ,kutofuata taratibu nzuri za
makusanyo yalikuwa yakitoka kwa wafugaji walipokuwa wakipata huduma za
kuongesha mifugo yao, hazikuwa na taarifa ya mapato na matumizi na hivyo
kushindwa kuwa na utaratibu endelevu wa shughuli hiyo, majosho mengi
yalisimama kufanya kazi"amesema Ulega
Katika
kampeni hii ya uhamamishaji wa uongeshaji wa mifugo tozo imepunguwa
ambapo hivi sasa kila ng’ombe ana ogeshwa katika majosho ni shilingi 50
tu, huko nyuma uogeshaji ulikuwa unatozwa wastani wa shilingi mia 2
kwa kila ngo’mbe na kwa mbuzi ilikuwa shilingi 10.
“Nyie
wafugaji msikalie rasialimali hii ya mifugo mliokuwa mnayo, kwani ni
uchumi mkubwa sana mliyokuwa nayo kwenu na pia kwa Taifa ili kuongeza
mapato, yanayotokana na mifugo yenu”amesisitiza Ulega.
Aidha
alifafanua kuwa ufungaji kwa kufuata taratibu za ufugaji wa kisasa na
kibiashara kwa kuvuna mifugo inapozidi katika eneo uliyokuwa nayo,
itakusaidia kupata kipato katika kuboresha maisha yako na ya familia.
Uhamasishaji
huu unafuatia uzinduzi wa kampeni ya uogeshaji wa mifugo,iliyofanywa na
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mh. Luhaga Mpina katikati ya mwezi jana
katika kijiji cha Buzirayombo halmashauri ya chato.
No comments:
Post a Comment