Diwani
wa kata ya Loiborsiret Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Ezekiel
Lesenga Mardad akizungumza kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa
Halmashauri hiyo kwa kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuwatetea
wafugaji hasa kijiji cha Kimotorok kjnachopakana na hifadhi ya jamii ya
Mkungunero.
Diwani
wa kata ya Terrat wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Jackson Ole Materi
akisoma taarifa ya hoja ya kumpongeza Rais John Magufuli kwa kuwatetea
wafugaji na watumishi wa serikali.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Yefred
Myenzi akisoma maazimio ya Baraza la Madiwani la kumpongeza Rais John
Magufuli kwa kuwatetea wafugaji na watumishi, kushoto ni Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Albert Msole.
Baadhi
ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara na
watumishi wa Halmashauri hiyo wakifuatilia kikao cha Baraza la
Madiwani.
Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, mhe
Albert Msole akifunga kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo
ambao walimpongeza Rais John Magufuli kwa kuwatetea wafugaji na
watumishi wa serikali, kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo
Yefred Myenzi.
Baraza
la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara,
limesoma maazimio ya kumpongeza Rais John Magufuli kwa kutatua migogoro
ya maeneo ya hifadhi na vijiji 366 na kurejesha kikokotoo cha awali cha
wastaafu.
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro, Yefred Myenzi akisoma maazimio hayo, alisema baraza hilo linampongeza kwa dhati Rais Magufuli kutokana na matukio hayo mawili.
Myenzi alisema baraza limeona maamuzi hayo ya Rais Magufuli ni kielelezo
tosha cha uongozi mahiri, uliotukuka na sikivu kwa wananchi wanyonge
ambao ni nguzo muhimu ya ujenzi wa Taifa.
Alisema uamuzi wa kurejesha kikokotoo katika utaratibu wa awali, ni kielelezo tosha cha uongozi mahiri na kutatua migogoro ya watumiaji wa ardhi na mipaka ya maeneo ya hifadhi ni ya kupongezwa.
"Kwa upendo huu aliouonyesha Mheshimiwa Rais Magufuli, baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro linampongeza kwa dhati na kuomba aendelee na moyo huu wa upendo kwa Taifa lake," alisema Myenzi.
Diwani wa kata ya Terrat, Jackson Ole Materi alisema mgogoro wa hifadhi na vijiji 366 ulikuwa unaathiri ustawi wa wananchi hasa jamii za wafugaji, wakulima, wavuvi na watumiaji wa ardhi katika mipaka ya vijiji na maeneo ya hifadhi.
Ole Materi alisema kwa uamuzi huo imedhihirika azma ya Rais Magufuli ya kuwajali wanyonge na kuhakikisha jamii yenye utulivu inayotumia muda mwingi kwa uzalishaji badala ya kutatua migogoro.
Diwani wa kata ya Loiborsiret, Ezekiel Lesenga (Mardad) alisema wananchi wa eneo hilo nao wanampomgeza Rais Magufuli kwa uamuzi wake kwani nao ni waathirika wa ardhi. Mardad alisema kwenye kijiji cha Kimotorok kuna taasisi mbalimbali ikiwemo shule, zahanati, kanisa na makazi ya watu waliotakiwa kufukuzwa sababu ya kupakana na hifadhi ya jamii ya Mkungunero.
Makamu
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Albert Msole alisema baraza hilo
linaundwa na jamii ya wafugaji na wakulima linampongeza Rais Magufuli na
kumtakia maisha marefu na ufanisi kwenye majukumu yake.
Msole alisema wilaya ya Simanjiro nayo ni miongoni mwa wanufaika wa matamko hayo mawili kwani watumishi wa serikali wamenufaika na wafugaji pia wamefaidika.
Diwani wa kata ya Emboreet, Christopher Kuya alisema Rais Magufuli amejali maslali na matakwa ya wafanyakazi ambao walikuwa waathirika wakubwa pindi wakistaafu.
"Uamuzi
huu wa Rais Magufuli ni kielelezo tosha cha uongozi wake thabiti na
sisi madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Simanjiro tunampongeza mno,"
alisema Kuya.
No comments:
Post a Comment