Balozi
wa Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju (mwenye miwani) akiwa
na washiriki wengine katika Maonesho ya Utalii ya Kimataifa
yanayofanyika nchini Uholanzi kuanzia tarehe 9 hadi 13 Januari 2019.
Wageni mbalimbali wanatembelea banda la Tanzania ili kupata maelezo kuhusu vivutio vya uwekezaji nchini.
Banda
la Tanzania linatia fora kwa kutembelewa na idadi kubwa ya watu
wanaotaka kupata maelezo kuhusu fursa na vivutio vya utalii nchini.
Wageni katika banda la Tanzania.
Balozi
Kasyanju na washiriki wenzake wakiwa katika badna la Tanzania tayari
kuanza kazi ya kuuza vivutio vya utalii nchini Uholanzi.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Tanzania yatafuta Soko la Utalii Uholanzi
Taasisi za Serikali
na kampuni binafsi mbalimbali za utalii zipo nchini Uholanzi kushiriki maonesho
ya utalii ya kimataifa kwa lengo la kutafuta fursa mpya za soko la utalii nchini
humo.
Maonesho
hayo maarufu kama Holday Fair 2019 (Vakantiebeurs2019) yalianza tarehe 9
Januari na yatakamilika tarehe 13 Januari 2019, hufanyika kila mwaka katika mji
wa Utrecht na kushirikisha taasisi mbalimbali kutoka duniani kote.
Taasisi za
Serikali zinazoshiriki ni Bodi ya Utalii Tanznaia (TTB), Mamlaka ya Hifadhi za
Taifa (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA). Kwa upande wa kampuni
binafsi ni into Africa Eco Travel Ltd, Migada Adventures, Mbalaget Tented Camp
Ltd, Kili Fair Promotions Ltd, East Africa Camps na Makasa Tanzania Safaris.
Balozi wa
Tanzania nchini Uholanzi, Mhe. Irene Kasyanju amesema kuwa maonesho hayo ni fursa
adhimu kwa nchi kutangaza vivutio vya utalii ambapo kwa mwaka 2019, waandaji
kwa mara ya kwanza wametoa nafasi kwa Balozi za nje zilizopo nchini humo
kutangaza pia fursa za biashara na uwekezaji.
Balozi
Kasyanju ambao Ubalozi wake unashiriki katika maonesho hayo alieleza kuwa maonesho
hayo yataenda sanjari na Vakantiebeurs Travel Congress, Vakantiebeurs Consumer
Day na Vakantiebeurs Trade Day ambapo washiriki watapata fursa ya kupeana
taarifa muhimu kuhusu mwelekeo na maendeleo ya biashara ya utalii katika maeneo
mbalimbali duniani, vivutio vipya pamoja na kufanya biashara.
Ushiriki wa
Tanzania katika maonesho hayo utasaidia washiriki kukutana na wadau na
kuanzisha uhusiano wa kibiashara unaotarajiwa kufungua soko la utalii nchini
baada ya wadau hao kupata maelezo ya kutosha kuhusu vivutio vilivyopo nchini na
faida zake.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki,
Dodoma, Tanzania
11 Januari 2019
|
No comments:
Post a Comment