Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Selemani Jafo
(kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge (kulia)
wakati alipokagua eneo itakapojengwa Hospitali ya Uhuru katika kijiji
cha Maduma wilayani Chamwino.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha michoro ya majengo ya Hospitali ya
Uhuru inayotarajiwa kujengwa katika kijiji cha Maduma wilayani Chamwino
wakati alipokagua eneo hilo.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo (katikati) na Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Faustine
Ndugulile wakati alipokagua eneo itakapojengwa Hospitali ya Uhuru
katika kijiji cha Maduma wilayani Chamwino.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru Mzee, Meshack Njamasi, mmoja wa
wananchi waliotoa maeneo yao bure kwa serikali ili yatumike kwa ujenzi
wa Hospitali ya Uhuru katika kijiji cha Maduma wilayani Chamwino.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru Mzee, Job Mahogo, mmoja wa wananchi
waliotoa maeneo yao bure kwa serikali ili yatumike kwa ujenzi wa
Hospitali ya Uhuru katika kijiji cha Maduma wilayani Chamwino.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amekagua eneo la ujenzi wa hospitali ya Uhuru
lenye ukubwa wa ekari 109 lililoko katika wilaya ya Chamwino mkoani
Dodoma. Akizungumza
na wakazi wa kijiji cha Maduma wilayani humo leo mchana (Ijumaa,
Januari 18, 2019), Waziri Mkuu amesema uamuzi wa Serikali ya kijiji
hicho wa kutenga maeneo ya maendeleo ni wa kupigiwa mfano na vijiji vya
maeneo mengine.
“Uamuzi
wenu wa kutenga maeneo ya miradi ya maendeleo umekuwa na tija, ndiyo
maana Mheshimiwa Rais Magufuli aliposema ijengwe hospitali, hamkupata
shida sababu eneo tayari lilikuwepo. Ninawapongeza wazee waliojitolea
maeneo yao ili kuongeza kwenye eneo la hospitali,” amesema.
Wazee
waliotoa maeneo yao ni Mzee Meshack Njamasi (ekari 5.50), Mzee Jobu
Malogo (ekari 3.50) na Bw. Nehemia Mwikwi (ekari 4.50). Ekari 95.5
zilizobakia, zimetolewa na Seriakli ya kijiji hicho.
Waziri
Mkuu aliwataka wakazi wa wilaya ya Chamwino wasibweteke bali wajipange
na kila mmoja ajipange kufanya kazi kama ambavyo Rais Magufuli amekuwa
akihimiza. “Ujenzi wa mji wa Serikali unaoendelea hivi sasa ni fursa
kwenu. Na ujio wa hospitali hii ni fursa nyingine kwa wana-Chamwino hasa
kwa vile ujenzi wake utatumia mfumo wa force account ambao unatoa fursa
kwa wanajamii kushiriki kazi za miradi ya eneo husika,” amesema.
Waziri
Mkuu amesema ujenzi wa hospitali hiyo yenye hadhi ya wilaya ni
utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inayoelekeza wananchi
wapatiwe huduma za matibabu huko huko waliko. “Hadi sasa tumeshajenga
vituo vya afya 350 ili kusogeza huduma kwa wananchi na jumla ya
hospitali za wilaya 67, zinajengwa nchi nzima kwa mwaka huu,” amesema.
Mapema,
akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wakazi wa vijiji jirani, Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), Bw. Selemani Jafo alisema eneo la
ujenzi wa hospitali hiyo liko umbali wa kilometa mbili kutoka barabara
kuu ya Dar es Salaaam-Dodoma na kilometa tatu kutoka Ikulu ya Chamwino.
Naye,
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt.
Faustine aliwataka wakazi hao wachangamkie fursa hiyo kwa kusomba mawe,
mchango, maji na kwamba Kamati za usimamizi wa ujenzi zitapaswa
kusimamiwa na wanakijiji.
Aliwataka
wakazi hao wasiishie kwenye lengo la kuwa na hospitali ya wilaya, bali
walenge kujenga hospitali yenye hadhi ya mkoa kwa kadri bajeti
itakavyoruhusu.
Akitoa
taarifa kwa Waziri Mkuu, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk. Bilinith Mahenge
alisema ujenzi wa hospitali hiyo ni wa hadhi ya wilaya ikiwa na nyongeza
ya huduma za wagonjwa wa dharura na wagonjwa mahututi (Emergency
Department and Critical Care Unit).
No comments:
Post a Comment