Mamlaka
ya Majisafi na Majitaka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) imeanza
kuwasambazia maji wananchi wa Kata ya Wazo na vitongoji vyake ikiwa ni
utekelezaji wa ahadi iliyotoa jumapili Jan 13, 2019. DAWASA imewekeza na
imejenga tanki kubwa lenye uwezo wa kihifadhi lita milioni sita
itakayofanya wakazi wa kupata maji kwa kipindi chote bila mgao.
Akizungumza
na wananchi mara baada ya kumaliza kazi na kuwapatia wananchi maji,
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa amewaomba wasimamizi
wa vizimba (Maduka ya kuuzia maji) kuuza maji kwa tsh. 50 kwa ndoo na si
tsh. 100 kama ilivyokuwa awali. "Leo mnafurahi kufunguliwa maji ila
naomba muuze maji tsh. 50 kwa ndoo, sitaki kuona wananchi wanalalamika
eti bei kubwa, mimi ndiyo msimamizi naomba mtekeleze mkumbuke na kulipa
ankara zenu za maji ili DAWASA waweze kuwahudumia vyema," amesema.
Mwishoni
kwa wiki iliyopita DAWASA kupitia Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA
Mhandisi Cyprian Luhemeja mbele ya wananchi akiwemo Mkuu wa Wilaya
Kinondoni Daniel Chongolo, aliwaahidi wakazi wa kata ya Wazo na
vitongoji vyake kuanzia wiki hii maji watapata bila mgawo wowote.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia) akishuhudia
utokaji wa maji eneo la Kata ya Wazo mara baada ya kukamilika kwa tanki
kubwa litakalowapatia maji kwa kipindi cha mwaka mzima bila kukatika.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia) akiongea na wananchi waliojitokeza kuchota maji. Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia) akiongea na
wananchi waliojitokeza kuchota maji huku akitoa maelekezo ya kuuza maji
kwa tsh. 50 kwa ndoo tu. Maji yakitoka.
Waziri
wa Maji na Umwagiliaji Prof. Makame Mbarawa (mwenye kofia) akipata
maelezo toka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA Mhandisi Cyprian
Luhemeja.
Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG.
No comments:
Post a Comment