Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wajumbe wa Kamati Maalum
iliyoundwa na serikali ya kusimamia uboreshaji wa Channel ya Utalii ya
TBC ya Tanzania Safari Channel, Ofisini kwa Waziri Mkuu Mlimwa jijini
Dodoma
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshukuru Katibu, Mkuu, Ofisi ya Waziri
Mkuu (Sera na Uwekezaji), Bibi Doroth Mwaluko (kushoto) wakati
alipokabidhiwa Hati ya Usajili wa Channel ya Utalii ya TBC ya Tanzania
Safari Channel katika kakao cha kuboresha Channel hiyo alichokiitisha,
Ofisini kwake jijini Dodoma, Januri 16, 2019. Wapili kushoto ni Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Utangazaji Tanzania
(TBC), William Kallaghe na Watatu kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC,
Ayoub Ryoba.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Cheti cha Usajili wa Channel ya
Utalii ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ya Tanzania Safari
Channel baada ya kuzungumza na Kamati Maalum iliyoundwa na Serikali ya
Uboreshaji wa Channel hiyo, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini
Dodoma,Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Ayoub Ryoba.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akionyesha Cheti cha Usajili wa Channel ya
Utalii ya Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ya Tanzania Safari
Channel baada ya kuzungumza na Kamati Maalum iliyoundwa na Serikali ya
Uboreshaji wa Channel hiyo, Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini
Dodoma,Wengine kutoka kushoto ni Katibu Mkuu, Ofisi
ya Waziri Mkuu (Sera na Uwekezaji), Bibi Doroth Mwaluko, Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Utangazji Tanzania (TBC) William
Kallaghe na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Ayoub Ryoba. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya
Mamlaka ya Usimazi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Meja Jenerali
Mstaafu, Hamisi Semfuko baada ya kuzungumza na Kamati ya Maalum ya
Uboreshaji wa Channel ya Utalii ya TBC ya Tanzania Safari Channel,
Ofisini kwa Waziri Mkuu, Mlimwa jijini Dodoma.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa amepokea leseni ya usajili wa chaneli ya utalii ya
Tanzania Safari ambayo itaiwezesha kuoneshwa kwa umma bila ya malipo
yoyote (a must-carry channel) na wamiliki wa visimbusi.
Waziri
Mkuu amekabidhiwa leseni hiyo leo mchana kwenye kikao alichokiitisha ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma ambako
alitaka apewe mrejesho kutoka kwa wajumbe wa Kamati Maalum ya kusimamia
uboreshaji wa Chaneli ya Utalii (Tanzania Safari Channel).
Akikabidhi
leseni hiyo kwa Waziri Mkuu, Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayoub Rioba
amesema kukamilika kwa usajili huo kumeiwezesha chaneli hiyo ianze
kuonekana kwenye kisimbusi cha AZAM namba 109.
Akitoa
taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Dkt. Rioba amesema Kamati hiyo iliundwa
Desemba 21, mwaka jana na inajumuisha wajumbe kutoka taasisi ambata za
maliasili na utalii kutoka Tanzania bara na Zanzibar.
“Baada
ya kupata leseni, sasa hivi tunaonekana kwenye kisimbusi cha AZAM
chaneli namba 109 na pia kwenye intelsat ambako tutaweza kuonekana
kwenye nchi zote barani Afrika, sehemu kubwa ya bara la Ulaya na
Uarabuni,” amesema.
Mapema,
akichangia hoja kwenye kikao hicho, Mwenyekiti wa Mamlaka ya Usimamizi
Wanyamapori Tanzania (TAWA), Meja Jenerali (Mst.) Hamisi Semfuko alisema
chaneli hiyo inaweza kunufaika kwa kupata matangazo kutoka kwa wamiliki
wa mahoteli, makampuni ya kutoa huduma za utalii na wenye magari ya
utalii.
Naye
Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA, Dkt. Allan Kijazi alisema chaneli ya
Tanzania Safari imekuja katika wakati muafaka kwa kuwa itaongeza juhudi
za taasisi zao kutangaza vivutio vilivyopo nchini na hivyo kuongeza
idadi ya watalii wa ndani na wa nje.
No comments:
Post a Comment