Ataka kampuni ya Mzinga Holdings isimamiwe kwa karibu
Ahimiza tarehe ya mwisho ni Januari 31, mwaka huu
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Jengo la Wizara ya Maji wakati
alipokagua ujenzi wa Mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa jijini
Dodoma, Januari 17, 2019. Wanne kulia ni Waziri wa Maji, Profesa Makame
Mbarawa, Watano kulia ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi,
Vijana na Ajira, Anthony Mavunde na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Mji wa Serikali katika eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Januari 17, 2019.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Jengo la Ofisi ya Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)
wakati alipotembelea Ujenzi wa Mji wa Serikali kwenye eneo la Ihumwa
jijini Dodoma Januari 17, 2019. Watano kulia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais TAMISEMI, Selemani Jafo na watatu kulia ni Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua Ujenzi wa Mji wa Serikali kwenye eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Januari 17, 2019.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Kangi Lugola (kulia) wakati alipokagua ujenzi wa jengo la Ofisi za
Wizara hiyo katika Mji wa Serikali unaojengwa eneo la Ihumwa jijini
Dodoma, Januari 17, 2019. Wapili kulia ni Waziri wa Elimu, Sayansi ya
Tekinolojia, William Ole Nasha na kushoto ni Katibu wa Kikosi Kazi cha
Kitaifa cha Kuratibu Mpango wa Serikali wa Kuhamia Dodoma, Meshack
Bandawe.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa, akizungumza na Saidi Kiwape (kushoto) ambaye ni
fundi wa kusuka nondo wakati alipokagua ujenzi wa Jengo la Ofisi za
Wizara ya Nishati kwenye eneo la Ihumwa unapojengwa Mji wa Serikali
jijini Dodoma, Januri 17, 2019. Wapili kulia ni Waziri wa Nishati, Dkt.
Medard Kalemani, watatu kulia ni Naibu Waziri , Ofisi ya Waziri Mkuu,
Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde na kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa
Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujezi wa tangi la maji lenye uwezo wa
kuhifadhi lita milioni moja za maji kwa ajili ya kuhudumia Mji wa
Serikali unaojengwa katika eneo la Ihumwa jijini Dodoma, Januari 19,
2019. Katikati ni Katibu wa Kikosi Kazi cha kitaifa cha Kuratibu
Mpango wa Serikali wa Kuhamia Dodoma, Meshck Bandawe.
Zikiwa
zimepita siku 20 tangu akague ujenzi wa mji wa Serikali, Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa amesema ameridhishwa na ujenzi unaoendelea katika eneo
la Mji wa Serikali lililoko Ihumwa.
Hata
hivyo, amesema kampuni ya ujenzi ya Mzinga Holdings inahitaji
kusimamiwa kwa karibu zaidi ili ikamilishe ujenzi wa majengo yake kabla
ya Januari 31, mwaka huu. “Nitakuja kukagua kazi na kupokea funguo za
ofisi siku hiyo,” amesema.
Ametoa
kauli hizo mara baada ya
kukagua ujenzi wa ofisi za wizara zote pamoja na Ofisi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali katika eneo la Ihumwa lililoko km. 17 kutoka jijini
Dodoma.
Waziri
Mkuu ambaye alianza kukagua ujenzi kwenye Ofisi ya Makamu wa Rais,
ametembelea majengo ya wizara zote na kubaini bado kuna changamoto
zinazojitokeza kutokana na utendaji wa mazoea miongoni mwa watumishi wa
Serikali.
Akiwa
katika jengo la Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Waziri Mkuu
alipokea malalamiko kutoka kwa meneja mradi, Bi. Selemina Rwehumbiza
kwamba aliandaa certificate tangu tarehe 13 Januari lakini hadi sasa
hajapata malipo. Alipofuatilia, alijibiwa na mshauri mwelekezi kwamba
wamepokea certificate hiyo jana jioni (Jumatano, Januari 16, 2019).
“Kama
kazi hii muhimu ya Mheshimiwa Rais, na anayesimamia ni Waziri Mkuu
inacheleweshwa hivi, je akija mwananchi wa kawaida huko ofisini kwenu
atachukua muda gani kupatiwa huduma?,” Waziri Mkuu alimhoji Mshauri
Mwelekezi wa mradi huo kutoka Wakala wa Majengo (TBA), Mhandisi Hilary
Msaki.
“Huu
ni mfano halisi wa malalamiko yanayotoka huko nje kwamba Serikali
haijibu barua za wananchi. Sasa nyaraka kutoka hapa Mtumba inachukua
wiki nzima kwenda mjini, na mtu bado hajajibiwa. Sielewi ni kwa nini
barua iende hadi mjini, wakati wakandarasi wako huku. Kwa nini ninyi
msipokee hizo nyaraka na kuzikimbiza mjini kisha mrudishe majibu hapa
site?”, alihoji Waziri Mkuu.
“Kuanzia
sasa, kazi zote mpokee ninyi, na ninyi ndiyo mzipeleke huko mjini na
kurudi na majibu hapa site kwa wateja wenu, kwani wakandarasi wote wako
hapa,” alisisitiza.
Akiwa
katika eneo la Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Waziri Mkuu alielezwa na Waziri Ummy Mwalimu kwamba wana
changamoto ya kutopatiwa taarifa za maendeleo ya mradi. “Tangu mradi
unaze hatujapewa taarifa hata moja, wakurugenzi wapo wanakuja, lakini
mshauri mwelekezi hatupi ripoti yoyote juu ya huu mradi,” alisema.
Alipohoji
ni kwa nini taarifa hazitolewi, Waziri Mkuu alibaini kuwa hata watu wa
TEMESA pia hawakuwepo kwenye zoezi hilo la ukaguzi. “Niliagiza TBA
wahamie hapa, nao wameweka ofisi yao hapa hapa. Nimeulizia Wakala wa
Ufundi na Umeme (TEMESA) wako wapi, nikaambiwa wako mjini. Ni kwa nini
hawako hapa?” alihoji.
Akizungumza
baada ya kukagua ujenzi wa tangi la maji lenye ujazo wa lita milioni
moja, Waziri Mkuu alisema pamoja na spidi anayoihimiza, bado wakandarasi
wanapaswa kufanya kazi kwa kuzingatia ubora unaotakiwa (quality).
Alisema
kwa ujumla kazi nyingi zimeboreshwa tangu alipokagua mradi huo Desemba
27, mwaka jana. Aliitaka TBA kwa kushirikiana na Kamati ya Kitaifa ya
kuratibu zoezi la Serikali kuhamia Dodoma na Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa/Mkurugenzi wa Dodoma wawasimamie wakandarasi na hasa wale wa Mzinga
ili kazi yao ikailike kwa wakati.
“Nimesisitiza
katika kila site, zile kazi ndogondogo zisizohitaji ujuzi au ufundi
mkubwa, zigawiwe kwa vijana ili kuongeza kasi lakini tuzingatie ubora wa
kazi,” alisisitiza.
Desemba
27, mwaka jana, Waziri Mkuu alikagua ujenzi wa eneo la Mji wa Serikali
na kubaini kuwa baadhi ya wakandarasi hawaendi na kasi inayotarajiwa na
Serikali. Siku iliyofuata aliitisha kikao cha Mawaziri wote, Makatibu
Wakuu na wakandarasi wao ili waeleze kazi hiyo itakamilishwa lini. Kikao
hicho alikifanyia hukohuko Ihumwa.
No comments:
Post a Comment