Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
amesema vituo vya afya 350 vitakuwa vimekamilika nchi nzima ndani ya
miaka mitano ya Uongozi wa Awamu ya tano
Makamu
wa Rais ameyasema hayo leo wakati alipotembelea kituo cha afya cha
Sokoine wilayani ya Singida mkoa wa Singida ikiwa muendelezo wa ziara
yake ya kikazi ambapo amekuwa akikagua na kuhamasisha shughuli za
maendeleo.
“Kulikuwa
na hospitali 65 za wilaya lakini tulivyoingia madarakani zimejengwa
hospitali 67 na lengo kuu ni kuwapa wananchi huduma bora ya afya”
alisema Makamu wa Rais.
Aidha
Makamu wa Rais alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Tano haitokubalina
na misaada ya masharti na imejidhatiti kufanya miradi ya maendeleo kwa
kutumia fedha zake za ndani.
Pamoja
na mambo mengine Makamu wa Rais alizindua barabara ya Karume ambayo
inajumuisha mradi wa mtandao wa barabara wenye urefu wa kilomita 6.1
ambazo nibarabara ya Karume yenyewe , Boma Kinyeto, Double Road Junction
(Semali Singida-Dodoma ).
Sambamba
na hayo, Mheshimiwa Makamu wa Rais alitembelea kituo cha afya Migori
ambapo alijionea maendeleo ya ujenzi ambao unatazamiwa kukamilika
mwishoni mwa mwezi machi, pia alitembelea shule ya sekondari ya
Mwanamema Shein ambapo alizungumza na wanafunzi na kujionea maendeleo ya
ujenzi wa bweni la wanafunzi pamoja na kupanda mti wa kumbukumbu.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipata maelezo ya maendeleo ya ujenzi wa kituo cha afya Migori wilayani
Singida kutoka kwa Kaimu Mhandisi wa Wilaya Dayness Rwehumbiza. Kituo
cha afya cha Migori ni moja ya vituo vilivyopata shilingi milioni 400 za
kitanzania. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akisalimia na Mkuu wa Sule ya Sekondari ya Mwanamema Shein Bi. Zainab
Mtindu wakati akiwasili kwenye shule hiyo iliyopo Migori, wilayani
Singida.
Wanafunzi
wa Shule ya Sekondari ya Mwanamema Shein iliyopo Migori wilayani
Singida wakiimba wimbo maalum wa kumkaribisha Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye yupo ziarani
mkoani Singida.
Naibu
Waziri wa Maji Mhe. Juma Awesu akizungumza na wanafunzi wa shule ya
sekondari ya Mwanamema Shein iliyopo Migori, Singida ambapo aliwasihi
wasome kwa bidii ili waje kuwa viongozi bora.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiweka udongo kwenye mti wa kumbukumbu alioupanda katika shule
ya sekondari ya Mwanamema Shein iliyopo Migori wilayani Singida.
Naibu Waziri Ujenzi Mhe. Elias Kwandikwa akizungumza wakati wa hafla
fupi ya kuweka jiwe la msingi wa ufunguzi wa barbara ya Karume iliyopo
Singida mjini ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ndio alikuwa
mgeni rasmi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza wakati wa hafla fupi ya kuweka jiwe la msingi wa ufunguzi wa
barbara ya Karume iliyopo Singida mjini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiweka jiwe la msingi kwenye ufunguzi
No comments:
Post a Comment