Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed
Shein, kulia Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein,
wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Bi,
Maryam Juma, Mabodi akitowa taarifa ya kitaalam wakati wa ziara yake
kukagua shimo la uchimbaji wa Mchanga la Pangatupu na Chechele Wilaya ya
Kaskazini B Unguja.kushoto kwa Katibu Waziri wa Ujenzi Mawasiliani
na Usafirishaji Mhe.Dr, Sira Ubwa Mwamboya.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali
Mohamed Shein, akizungumza wakati wa ziara yake kutembelea bonde la
mchanga la Pangatupu na Chechele Wilaya ya Kaskaszini B Unguja,
kulia Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein, na kushoto Katibu
Mkuu Wizara ya Kilimo Maliasili Mifugo na Uvuvi Bi. Maryam Juma Mabodi,
Wasili wa Ujenzi Mawasiliano na Usafirishaji Mhe.Dr. Sira Ubwa Mwaboya
na Waziri wa Ardhi,Maji Nishati na Makaazi Mhe. Salama Aboud Talib,
wakifuatilia hafla hiyo.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein, akiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali
Iddi, wakitembelea Bonge la machimbo ya mchanga la Pangatupu Wilaya ya
Kaskazini B Unguja wakati wa ziara yake kukagua eneo hilo la uchimbaji
akiwa katika ziara yake, katika Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein, akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe. Vuai Mwinyi,
wakati akiwa katika ziara yake kutembelea mashimo ya uchimbaji wa
mchanga katika maeneo ya Pangatupu na Chechele Wilaya ya Kaskazini B
Unguja, muonekano wa nyuma ni eneo hilo lililokuwa likichimbwa
mchanga na kusimamisha uchimbaji wa mchana.katikati Waziri wa Nchi Ofisi
ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ
Mhe. Haji Omar Kheri.
Mbunge
Mstaaf wa Jimbo la Donge Ali Ameir Mohammed akiwa na Viongozi wa
Serikali na Chama wakati wa mkutano wa Majumuisho ya ziara ya Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein,katika Wilaya ya Kaskazini B Unguja, yaliofanyika katika ukumbi wa
hoteli ya Sea Cliff.
ENEO
la Panga Tupu na Chechele Jimbo la Bumbwini Shehia ya Kidazini,
lililosimamisha shughuli za uchimbaji wa mchanga, kama linavyoonekana
picha wakati wa ziara ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika ziara yake katika
Wilaya ya Kaskazini B Unguja, kujionea hali hiyo.
BAADHI
ya Waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali Zanzibar wakiwa katika
hafla ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.
Ali Mohamed Shein, alipotembelea mashimo ya Uchimbaji wa Mchanga katika
maeneo Pangatupu na Chechele Wilaya ya Kaskazini B Unguja leo,akiwa
katika ziara yake.
BAADHI
ya Vijana wanaofanya shughuli zao katika mashimo ya mchanga ya Panatupu
na Chechele wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein, alipotembelea eneo hilo akiwa
katika ziara yake katiuka Wilaya ya Kaskazini B Unguja.(Picha na Ikulu)
No comments:
Post a Comment