Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai
akizungumza Bungeni nakuiomba Serikali kutoa tamko kuhusu ambazo
imeshachukua kuhusu hali ya mauaji ya watoto Mkoani Njombe kabla ya
Bunge hilo kuhairishwa wiki hii.
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akijibu maswali mbalimbali ya wabunge Bungeni Jijini Dodoma.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe.Dkt.
Faustine Ndugulile akijibu hoja mbalimbali za Wabunge Bungeni
Jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
Angeline Mabula akitolea ufafanuzi hoja mbalimbali za wabunge
Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri
wa Katiba na Sheria Mhe.Palamagamba Kabudi akiteta Jambo na Waziri
wa Madini Mhe. Doto Biteko Bungeni Jijini Dodoma.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera,
Bunge, Kazi, Vijana na Wenye Ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Peramiho,
Jenista Mhagama, wakifuatilia mijadala inayo endelea Bungeni Mjini
Dodoma.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa mwenye suti nyeusi, akisalimiana na Mbunge wa
kuteuliwa, Abdalah Bulembo. kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma.
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mbunge wa Viti maalumu Mkoa wa
Shinyanga.Azza Hamad, Bungeni jijini Dodoma, Februari 4, 2019.
(Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
No comments:
Post a Comment