Frank Mvungi – MAELEZO, Dodoma
Mpango
wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA)
umepongezwa kwa kuwawezesha wananchi Wilayani Chamwino mkoani Dodoma kwa
kuwajengea uwezo ili waweze kutumia hati za kimila za kumiliki ardhi
kujiletea maendeleo.
Akizungumza
leo Wilayani humo wakati akifungua mafunzo kwa wakulima zaidi ya 100
wa Kijiji cha Membe mbunge wa jimbo hilo Mhe. Joel Mwaka amesema kuwa
wananchi wanajengewa uwezo ili waweze kutumia hati hizo kujiletea
maendeleo ikiwemo kuzitumia kama dhamana kuchukua mikopo katika Taasisi
za fedha kama mabenki.
“
Nawapongeza Ofisi ya Rais- MKURABITA kwa kuwezesha mashamba 1145
kupimwa na tayari hatimiliki za kimila 1000 zimeweza kuandaliwa ili
kuwawezesha wananchi kuzitumia kujikwamua kiuchumi” Alisisitiza Mwaka.
Akifafanua
amesema kuwa kuna umuhimu wa kuunga mkono juhudi za MKURABITA kwani
kati ya vijiji 107 vilivyopo katika halmashauri hiyo ni viwili tu
vimebahatika kupata fursa ya kurasimishiwa ardhi na kujengewa uwezo
kupitia mafunzo yanayoendeshwa na mpango huo kwa kushirikiana na
Halmashauri ya Wilaya hiyo.
Aliongeza
kuwa kuna umuhimu mkubwa kwa wananchi kujitokeza kuchukua hati zao ili
wazitumie kujikwanua kiuchumi kwa kuwa zimeshandaliwa na ziko tayari.
“
Faida za hati hizi ni pamoja na kuhakikisha usalama wa milki ya
mkulima, kuongeza thamani ya ardhi na pia itasaidia kukuza uchumi wa
Wilaya ya Chamwino na Taifa kwa ujumla” Alisisitiza Mwaka.
Alibainisha
kuwa wakulima hao zaidi ya 100 watakuwa chachu ya kutosha kwa Wilaya
hiyo na kuleta mabadiliko makubwa katika uzalishaji kwenye kilimo na
ufugaji na hivyo kuongeza tija na kipato kwa wakulima wilayani humo.
Kwa
upande wake Mratibu wa MKURABITA Bi. Seraphia Mgembe amesema kuwa
Dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha kuwa wanachi
wanajikwamua kiuchumi kupitia uwezeshaji unaofanywa kwa kurasimisha
mashamba ya wananchi na kuwapa hati ili waweze kuzitumia kujiletea
maendeleo.
“
Mkitumia hati hizi vizuri kama Serikali ilivyodhamiria mtajikwamua
kichumi kwani hapa kila aliyepewa tayari ajihesabu kuwa yeye ni mmiliki
wa ardhi yenye thamani na inayoweza kuleta mageuzi makubwa katika maisha
yake” Alisisitiza Bi. Mgembe.
Akifafanua
zaidi amesema kuwa ni vyema wananchi wakaepuka vitendo vya kuuza ardhi
zao kiholela badala yake wazitumie kwa tija hata pale wanapoamua kuuza
sehemu ya maeneo yao walenge kujiletea maendeleo ili kuendana na dhana
ya kujenga uchumi jumuishi inayosisistizwa na Serikali .
MKURABITA
itaendesha mafunzo hayo kwa siku tatu yakilenga kuwajengea uwezo
wakulima wa kijiji cha Membe kuzalisha kwa tija kupitia kilimo cha
alizeti, ufugaji na pia watapata kujengewa uwezo kuhusu namna ya kutunza
kumbukumbu, utafutaji fursa na namna ya kuzitumia, uandishi wa mpango
wa biashara na uundaji wa vikundi vya hiari, utunzaji wa kumbukumbu na
uthamini wa ardhi na utunzaji wa mazingira.
Mbunge
wa Jimbo la Chamwino Mhe. Joel Mwaka akifungua mafunzo kwa wakulima
waliorasimisha mashamba yao na kupata hati za kimila za kumiliki ardhi
kupitia Ofisi ya Rais, Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za
Wanyonge Tanzania (MKURABITA) leo Wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Mratibu
wa MKURABITA Bi. Seraphia Mgembe akisisitiza umuhimu wa wananchi
kutumia hati za kimila za kumiliki ardhi kujiletea maendeleo wakati wa
ufunguzi wa mafunzo yakuwajengea uwezo wakulima zaidi ya 100 wa vijiji
vya Membe na Mahama Wilayani Chamwino mkoani Dodoma.
Meneja
urasimishaji ardhi vijijini kutoka MKURABITA Bw. Antony Temu akieleza
faida za mafunzo yakuwajengea uwezo wakulima wa Wilaya ya Chamwino
katika Kijiji cha Membe ili waweze kutumia hati milki za kimila za
kumiliki ardhi walizopata kujiletea maendeleo.
Mratibu
wa MKURABITA Bi. Seraphia Mgembe akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa
Kijiji cha Membe Bw. Yoram Majenda leo Wilayani Chamwino mara baada ya
ufunguzi wa mafunzo kwa wakulima zaidi ya 100 na viongozi 10 yakilenga
kuwajengea uwezo wa kutambua fursa zilizopo baada ya kurasimisha
mashamba yao na kupata hati milki za kimila za kumiliki ardhi.
Mbunge
wa Jimbo la Chamwino mkoani Dodoma Mhe. Joel Mwaka akiwa kwenye picha
ya pamoja na sehemu ya wananchi waliopatiwa hati za kimila za kumiliki
ardhi baada ya kurasimisha mashamba yao katika Kijiji cha Membe.
Sehemu
ya wanachi walioshiriki hafla ya kufungua mafunzo kwa wakulima zaidi ya
100 na viongozi 10 katika kijiji cha Membe wilayani Chamwino mkoani
Dodoma wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la
Chamwino mkoani Dodoma Mhe. Joel Mwaka Wilayani humo.
(Picha zote na MAELEZO)
No comments:
Post a Comment