Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar amesema kuwa siasa za
vyama vingi zimekuja kwa lengo la kushidana kwa Sera na sio
kukashifiana.
Katika hotuba yake Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Rais Dk. Shein alisema kuwa siasa za vyama vingi havikuja kwa lengo baya la kukashifana na badala yake vina lengo zuri la kushindana kwa Sera ili iwe kivutio kwa wanachama na sio ugomvi.
Hivyo, Rais Dk. Shein aliwasisitiza wananchi wa Wilaya hiyo kuishi kwa mapenzi na kufahamiana sambamba na kushirikiana pamoja kwao wote ni ndugu.
Aidha, Makamu huyo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar aliwataka viongozi wa CCM kutembelea Matawi, Wadi, Majimbo na Wilaya zao sambamba kuwatembelea wananchi na wanachama wa chama chao ili kuwasikiliza changamoto walizonazo na kuzitafutia ufumbuzi.
Pia, Rais Dk. Shein aliwataka viongozi wa CCM wa Wilaya hiyo kuimarisha miradi ya ili chama hicho kiweze kupata mapato ya kuweza kukiimarisha na kuapata mafanikio makubwa zaidi.
Rais Dk. Shein alieleza kuwa tayari utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2015-2020 imeshatekelezwa kwa kiasi kikubwa na ahadi nyingi zilizoahidiwa zimeshatekelezwa sambamba na zile ambazo haziko katika Ilani.
Alisisitiza kuwa viongozi wote waliomo Serikalini ni vyema wakatambua kuwa wanatekeleza Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha CCM, hivyo, wanakila sababu kufanya kazi zao kwa bidii na yule ambaye hatoweza anapaswa kukaa pembeni.
Aliongeza kwua huo ni utaratibu wa Serikali zote duniani kwa chama kinachoongoza Serikali ni lazima viongozi wote watekeleze Ilani ya Chama hicho kwani ndicho kilicho madarakani na ndicho kinachoongoza nchi.
Rais Dk. Shein alieleza kuwa huo ndio utaratibu wa kimataifa na demokrasia ya nchi hivyo viongozi wote waliomadarakani katika Serikali anayoiongoza hawana budi kutekeleza Ilani ya CCM kwani ndicho chama kilicho madarakani,
Alieleza kuwa ujenzi wa barabara ya Mkanyageni- Kangani (Km 6.5) ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020 ambayo imetajwa katika Ilani hiyo kwenye ukurasa wa 149.
Aidha, ujenzi wa jengo la skuli ya Sekondari Michenzani, Mkoani Pemba pia ni utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi katika kuimarisha sekta ya elimu Zanzibar.
Ambapo pia, Rais Dk. Shein alieleza azma ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya CCM ya kujenga barabara ya Chake hadi Mkoani yenye (Km 27), ambayo hivi sasa imo katika mchakato wa michoro.
Rais Dk. Shein pia, aliusisitiza uongozi wa CCM wa Mkoa na Wilaya hiyo kuimarisha historia ya ASP kwa kulijenga jengo la Tawi la CCM lenye historia ya ASP huko Mkanyageni ambalo lilitumika na wazee waasisi kama vile marehemu mzee Mohamed Juma Pindua na yeye kuahidi kuchangia mabati kwa ajili ya ujenzi huo.
Sambamba na hayo, Rais Dk. Shein alizipongeza taarifa zilizotolewa mbele yake ikiwemo taarifa ya Serikali ya Wilaya ya Mkoani pamoja na taarifa ya Chama iliyotolewa na uongozi wa CCM Wilaya ya Mkoano.
Rais Dk. Shein pia, aliupongeza uongozi wa CCM Wilaya hiyo ya Mkoani kwa kuongeza idadi ya wanachama sambamba na ulipaji wa ada kwa wanachama wa chama hicho.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed
Shein, na Mama Mwanamwema Shein, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Mmanga Mjengo Mjawiri, wakiwa katika moja
ya madarasa ya Skuli hiyo ya Sekondari ya Michezani baada ya ufunguzi
wake ,likiwa na meza na viti vipya vilivyoagizwa na Serikali kwa Skuli
za Sekondari na Msingi Zanzibar.(Picha na Ikulu)
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein, akihutubia wakati hafla ya Uzinduzi wa Madarasa ya Skuli ya
Sekondari ya Michezani Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba, akiwa katika
ziara yake kutembelea Mikoa ya Kusini na Kaskazini Pemba kuangalia
miradi ya Maendeleo.(Picha na Ikulu)
NAIBU
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.Bi. Madina
Mjaka, akitowa Taarifa ya Kitaalam ya ujenzi wa Madarasa ya Skuli ya
Sekondari ya Michezani Wilaya ya Mkoani Pemba wakati wa hafla hiyo ya
uwekaji wa jiwe la msingi leo.(Picha na Ikulu)
/WANAFUNZI
wa Skuli ya Michezani Wilaya ya Mkoani Pemba wakifuatilia hutuba ya
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali
Mohamed Shein. hayuko picha wakati wa hafla ya uzinduzi wa Skuli ya
Sekondari ya Michezani leo, 21-2-2019.(Picha na Ikulu)
WANANCHI
wa Kijiji cha Michezani Wilaya ya Mkoani Pemba wakimsikiliza Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein,akihutubia wakati wa hafla ya uzinduzi na uwekaji wa jiwe la
msingi Skuli ya Sekondari ya Michezani Pemba.
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed
Shein, akimpongeza Mwanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Michezo baada ya
kumaliza kusoma Quran Surat Afaq Mwanafunzi Salim Shehe Hussein, kulia
kwa Rais Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Mmanga
Mjengo Mjawiri na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein.
BAADHI
ya Viti na Meza Mpya vilivyoagizwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar
kwa ajili ya Skuli za Sekondari na Msingi Zanzibar, tayari vimeshagawiwa
kwa Skuli za Sekondari za Unguja na Pemba, kwa ajili ya matumizi ya
Wanafunzi.
JENGO Jipya la Skuli ya Sekondari ya Michezani Kisiwani Pemba Wilaya ya Mkoani.(Picha na Ikulu)
No comments:
Post a Comment