Serikali
imesema kipaumbele kikubwa katika sekta ya elimu kwa sasa ni
kuhakikisha watoto wenye mahitaji maalum wanakuwa na mazingira salama na
rafiki katika mchakato wa kujifunza ili kuwawezesha kupata elimu bora.
Kauli
ya Serikali imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu,
Sayansina Teknolojia Dkt. Ave Maria Semakafu wakati akifunga mkutano wa
kimataifa wa kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mradi wa
Girls Inspire wenye lengo la kuzuia ndoa za utotoni uliofanyika Jijini
Dar es Salaam.
Naibu
Katibu Mkuu huyo amesema kundi la watoto wenye mahitaji maalum
linasaulika hata unapoangalia miradi ya elimu inayoletwa na wafadhili
mara nyingi inaangalia matatizo ya mimba au mila kandamizi lakini
wanasahaulika, kundi hili ambalo ni wahanga namba moja wa mila hizo
kandamizi ambazo zinawakosesha fursa ya kupata elimu.
“Watoto
wenye mahitaji maalum wanasaulika hata wenzetu wafadhili wanapokuja
kuanzisha miradi mara nyingi wanapenda kuongelea mambo ya mimba na mila
kandamizi lakini wanasahaulika kwamba kundi hili la watoto wenye
mahitaji maalum ambao unapoongelea mila kandamizi wao ni wahanga namba
moja haijalishi kama wamepata mimba lakini tumewawekea alama kutokana na
maumbile yao ” alisemaDkt. Semakafu.
Dkt.
Semakafu amesema Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansina Teknolojia
limeweka kipaumbele kwa kundi hili kwa kuhakikisha miundombinu ya shule
ambazo zinachukua watoto wenye mahitaji maalum zinapewa kipaumbele
katika kuboreshwa, kununua visaidizi vya watoto wenye mahitaji maalum
ili waweze kusoma na kupata elimu yao katika mazingira yaliyoboreshwa na
salama.
Aidha,
amesema kwamba mkaka ti mwingine wa serikali ni kuhakikisha kila mkoa
unakuwa na shule maalum kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalum ili
kuwezesha kuwalinda watoto bora kama watoto
wengineiliwawezekujisaidiakatikamaishayaoyabaadaye.
Naye
Mkurugenzi Mkuu na Rais wa Kitengo cha Elimu la Jumuiya ya Madola
(COL), Profesa Asha Kanwaramwe ataka washiriki wanaoutekeleza muda huo
kutoa chakuutekeleza kwasababu yeyote ile kwani unadabadili maisha ya
wasichana wengi nakutaka nchi ishiriki kuimarisha elimu masafa ambayo
imekuwa msaada mkubwa kwa wasicha na wanaopata mimba.
Mradiwa
Girls Inspire unalenga kuzuia ndoa za utotoni unatekelezwa katika nchi
za Tanzania, Msumbiji, Bangladesh, India na Pakistani na kufadhiliwa na
serikali za Canada na Australia ambapo kwa Tanzania umatekelezwa na
Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Shirika lisilo la Serikali Kiota
Women Health and Development, (KIHOWEDE).
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansina Teknolojia Dkt. Ave Maria
Semakafu akifunga mkutano wa kimataifa wa kupokea na kujadili taarifa ya
utekelezaji wa mradi wa Girls Inspire wenye lengo la kuzuia ndoa za
utotoni uliofanyika Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkuu na Rais wa Kitengo cha Elimu la Jumuiya ya Madola (COL), Profesa
Asha Kanwaramwe akizungumza wakati wahafla ya kufunga mkutano wa
kimataifa wa kupokea na kujadili taarifa ya utekelezaji wa mradi wa
Girls Inspire wenye lengo la kuzuia ndoa za utotoni uliofanyika Jijini
Dar es Salaam. (Picha zote na TEW)
No comments:
Post a Comment