NA K-VIS BLOG/Khalfan Said, Morogoro
SERIKALI imekabidhi rasmi eneo la mradi wa umeme wa maporomoko
ya maji ya Mto Rufiji (RHPP), leo Februari 14, 2019 kwa mkandarasi Kampuni ya
Arab Contractors kwa pamoja na ile ya Elsewedy Electric zote kutoka nchini Misri.
Hatua hiyo sasa inaashiria kuanza kwa kazi ya ujenzi wa mradi
huo wa umeme ambao utazalisha Megawati 2,115 ambazo zitaingizwa kwenye dridi ya
Taifa na kuifanya Tanzania kuwa na umeme mwingi na wa uhakika.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mradi huo kwa mkandarasi
katika hafla iliyofanyika ndani ya Pori la Akiba la Selous, Waziri wa Nishati,
Dk. Medard Kalemani, amesema kuwa hatua hiyo inatokana na uamuzi wa Rais Dk.
John Magufuli kwa kusimamia uamuzi wa ujenzi wa mradi huo mkubwa.
Alisema mradi huo ulibuniwa kwa muda mrefu tangu mwaka 1970
ambapo kazi ya uchambuzi ilifanyika lakini haukutekelezwa kwa sababu ya gharama
zake kuwa kibwa.
"Wakati ule (1970), mahitaji ya umeme yalikuwa megawati
100. Lakini leo mahitaji ya umeme ni makubwa sana. Na ilipangwa kwa wakati ule
kutekelezwa kwa awamu ambapo ungeanza na megawati 400, awamu ya pili 800 na
baadaye megawati 900. Hatua tuliyofikia leo ndiko serikali ya awamu ya tano
inataka ya Tanzania ya viwanda
"Huu ni mradi wa manufaa miji yote iliyozunguka mradi huu
itakuwa kwa kasi sambamba na uzalishaji wa umeme," alisema
Waziri huyo wa Nishati, alisema kuwa mkandarasi Arab
Contractors, atafanyakazi ya kujenga bwawa la umeme ikiwamo kingo za kuta
pamoja na kujenga vituo ya kuzalisha umeme.
"Ninapenda mtekeleze mradi huu kwa wakati na kwa ufanisi
ili kuondoa mashaka kwa watu ambao wenye shaka. Leo mnakabidhiwa eneo la kazi
ni matumaini yetu itaifanyakazi hii kwa wakati ili wananchi waweze kunufaika na
umeme.
"Na kuanzia leo (jana) wakandarasi msiondoke site nyumba
zipo, miundombinu ipo iwe jua, mvua jengeni mradi wakati wote na msiondoke
hapa," alisema
Alisema pia kitajengwa kituo cha kupoza na kukuza umeme cha kV
400 na njia za kusafirisha umeme kwa msongo wa kV 400 kutoka eneo la
mradi hadi Chalinze kwenda Dodoma na Dar es Salaam na utakamilika mwaka 2022.
MANUFAA YA MRADI
Dk. Kalemani, alitaja manufaa ya mradi huo ikiwamo kuifanya nchi
kuwa na umeme wa uhakika na wa kutosha utakaosaidia maendeleo ya uchumi wa
viwanda na maendeleo endelevu ya wananchi.
Mbali na hiyo pia nchi itakuwa na maji ya uhakika kwa ajili ya
kilimo cha umwagiliaji hivyo kuongeza uzalishaji wa mazao na ufugaji kwenye
eneo lililo chini ya eneo la mradi wa maporomoko ya Mto Rufiji.
"Kuboresha shughuli za utalii katika Pori la Akiba la
Selous kwa kuwapo mazingira mazuri ya ustawi wa wanyama pori kutokana na
uhakika wa maji wakati wote ya bwawa litakalotokana na ujenzi wa mradi.
"Kuongeza mapato ya nchi kutokana na kustawi kwa shughuli
za kitalii katika eneo la mradi. Kuvutia uwekezaji katika sekta ya viwanda na
sekta mbalimbali za uchumi kutokana na kuwepo kwa umeme wa uhakika na wa bei
nafuu hivyo kupunguza tatizo la ajira.
"Kupunguza athari za mafuriko ya Mto Rufiji kwa wakazi
waliopo maeneo ya Rufiji chini hadi delta ya Mto Rufiji na kuongeza pato la
Taifa na lishe kutokana na mazao ya uvuvi," alisema Dk. Kalemani.
MAKAMU WA RAIS ARAB
Kwa upande wake Makamu wa Rais wa Kampuni ya Arab
Contractors, Wael Hamdy, alisema umuhimu wa mradi huo si kwa Tanzania tu
bali ni kwa Afrika kwa ujumla.
Alisema kwa niaba ya Serikali ya Misri, watahakikisha
wanatekeleza mradi huo kwa si mara ya kwanza kupingwa kwani hata walipoteleleza
ujenzi wa Bwawa la Azuan, walipingwa na mataifa mengine lakini Tanzania kupitia
Mwalimu Julius Nyerere, aliwaunga mkono Misri.
"Hata kazi ya kupata zabuni ya mradi huu haikuwa kazi
nyepesi lakini tunaamini kwa usimamizi wa Rais Dk. John Magufuli, tunaiona
Tanzania ikiwa kwenye mwekeo sahihi. Na katika hili linadhirisha hata mwaka
jana nilipofika hapa Tanzania na Rais Abdufatah Al-sis, ninaiona Tanzania leo
ikiwa imepiga hatua kubwa hapa ni kazi tu," alisema Hamdy
WIZARA YA FEDHA
Akitoa salamu za Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango,
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Dk. Ashatu Kijaji, alisema kuwa wao kama wizara
ambao ni wadau muhimu kwenye utekelezaji watatoa ushirikiano wa kila aina
unaohitajika ili kazi ikamilike kwa wakati.
"Haya matunda ya Serikali ya awamu ya tano sote tunajua
wapi tulipotoka, tulipo na tunapokwenda. Na tunajua sasa tupo kwenye
utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Taifa Awamu ya pili ambao hadi kufikia
mwaka 2025 tunataka kuwa Tanzania inayotekegea uchumi wa kati na wa viwanda. Na
utekelezaji wa mradi huu tunaambiwa hakuna viwanda bila umeme na mradi huu sasa
unakwenda kulifanya Taifa kuwa na umeme mwingi na wa uhakika zaidi,"
alisema Dk. Kijaji
DK. MWINUKA
Awali akitoa maelezo kuhusu mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika
la Umeme Tanzania (Tanesco), Dk. Tito Mwinuka, alisema kuwa ujenzi huo
utajumuisha bwawa kuu aina ya Rollar Compacted lenye uwezo wa kutunza maji
takribani mita za ujazo bilioni 34, kituo cha kufua umeme zenye uwezo wa MW
2,115.
"Aidha patajengwa majengo ya ofisi, karakana, makazi, stoo
na huduma za jamii kwa ajili ya uendeshaji wa kituo," alisema
Alisema zabuni ya kumpata mkandarasi wa ujenzi ilipelekea
kuipata Kampuni ya ubia ya Arab Contractors ambayo inaundwa na kampuni za Osman
A. Osman & Co na Elsewedy Electric zote kutoka nchini Misri.
Mkurugenzi huyo Mtendaji alisema katika kutekeleza mradi huo
kutakuwa na mtaalamu mshauri wa mradi kwa ajili ya kuangalia ubora wa utendaji
kazi wa mkandarasi kwa kushirikiana na timu ya timu ya wazalendo kwa niaba ya
mwenye mradi.
Alisema baada ya kusainiwa kwa mradi huo kuna mambo ambayo
mkandarasi alitakiwa kuyafanya na amekamilisha kwa mujibu wa masharti ya
mkataba.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani,
akibadilishana mawazo na naibu waziri wa Nishati, Mhe.Subira Mgalu,
(wapili kulia) Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji,
(watatu kulia) na Mkurugenzi Mtedaji wa Shirika la Umeme Tanzania
TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka muda mfupi baada ya hafla hiyo.
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani,
(katikati) akisindikizwa na manaibu waziri na wakandarasi, akikata
utepe ikiwa ni ishara ya kukabidhi rasmi mradi wa ujenzi wa kuzalisha
umeme wa bonde la Mto Rufiji leo Februari 14, 2019.
Mratibu wa Mradi wa umeme wa Rufiji
Mhandisi Justus Mtolela (waliokaa kulia) na mwakilishi wa mkandarasi
Mhandisi Ahmed Ouda wakisaini mkataba wa makabidhiano ya eneo la mradi
tayari kuanza kazi. Hafla hiyo iliyoshuhudiwa na Waziri wa Nishati, Dkt.
Medard Kalemani manaibu waziri na viongozi mbalimbali wa serikali
ilifanyika eneo la mradi wilayani Rufiji leo Februari 14, 2019.
Mratibu wa Mradi wa umeme wa Rufiji Mhandisi Justus Mtolela(kulia) na Mhandisi Ahmed Ouda, wakionyesha hati hizo baada ya ksuaini. |
Makamu wa Rais wa kampuni ya Elsewedy Electric ya Misri, Mhandisi Wael Hmdy, akitoa hotuba yake
Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani akitoa hotuba yake kwa niaba ya Serikali.
Mbunge wa Rufiji Mhe.Mohammed Mchengerwa, akitoa hotuba.
Dkt. Kalemani akisalimiana na Naibu
waziri wake, Mhe. Subira Mgalu, Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt.
Ashatu Kijaji, na Naibu Waziri wa Maliasili Costantine Kanyasu, mara
baada ya hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt.
Tito Mwinuka, (kushoto), akijadiliana jambo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji
wa Shirika hilo anayeshughulikia uwekezaji, Mhandisi Khalid James, mara
baada ya hafla hiyo.
Sehemu ya Mto Rufiji mahala ambapo payajengwa bwawa kubwa la maji ya kufua umeme
Baadhi ya wataalamu wa Serikali walioshiriki kwenye mchakato wa mwanzo wa kuanza kwa uchambuzi wa mradi huo wakijumuika pamoja na viongozi wa wilaya zinazopakana na mto Rufiji.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Bw. Waziri
Kindamba (kushoto), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito
Mwinuka
Manaibu Wazoiri kutoka kulia, Mhe.
Subira Mgalu (Nishati), Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Fedha na Mipango) na
Mhe. Costatine Kanyasu (Maliasili na Utalii, wakati wakichukua nafasi
zao kwenye eneo la tukio,
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Dkt. Hamisi Hassan Mwinyimvua
(akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO anayeshughulikia
uwekezaji, Mhandisi Khalid James, wakati akiwasili eneo la tukio,
wanaoshuhudia ni Dkt. Tito Mwinuka (wapili kushoto) na Mbunge wa Rufiji
Mkoani Pwani, Mhe. Mchengerwa (kulia).
Baadhi ya wataalamu wa Serikali walioshiriki kwenye mchakato wa mwanzo wa kuanza kwa uchambuzi wa mradi huo wakijumuika pamoja na viongozi wa wilaya zinazopakana na mto Rufiji.
No comments:
Post a Comment