Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Balozi wa Kuwait
nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan (kulia), juu ya kubadilishana
uzoefu katika Udhibiti wa Mipaka. Mazungumzo hayo yamefanyika leo,
Ofisi Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Balozi wa Kuwait nchini, Mubarak
Mohamed Alsehaijan, akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni juu ya kubadilishana uzoefu katika
Udhibiti wa Mipaka.Mazungumzo hayo yamefanyika leo, Ofisi Ndogo ya
wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Balozi wa Kuwait Nchini, Mubarak
Mohamed Alsehaijan akisaini Kitabu cha Wageni baada ya kuwasili Ofisi
Ndogo ya Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, jijini Dar es Salaam. Kushoto
ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mhandisi Hamad Masauni.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akiagana na Balozi wa Kuwait nchini,
Mubarak Mohamed Alsehaijan (kulia), baada ya kumaliza mazungumzo
yaliyohusu kubadilishana uzoefu katika Udhibiti wa Mipaka.Mazungumzo
hayo yamefanyika leo, Ofisi Ndogo ya wizara, jijini Dar es Salaam.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Serikali ya Tanzania na Nchi ya
Kuwait ziko katika mpango maalumu wa kubadilishana uzoefu juu ya
udhibiti wa mipaka ikiwa ni juhudi za Tanzania kuimarisha ulinzi katika
mikoa yote nchini iliyopo mipakani
Hayo yamebainishwa na Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni wakati wa
mazungumzo na Balozi wa Kuwait Nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan ikiwa
ni mpango wa nchi hizo kubadilishana uzoefu katika kudhibiti uhalifu
katika mikoa ya mipakani
“Kama Serikali tuna vipaumbele
katika kudhibiti mipaka yetu kutokana na uhalifu unaotokea ikiwemo
wahamiaji haramu,usafirishaji wa binadamu, uingiaji wa
silaha,utoroshwaji wa madini na biashara yamagendo, ndio maana
tumekutana leo kujadili ushirikiano wa nchi hizi mbili katika kudhibiti
uhalifu huo”alisema Masauni
Akizungumza katika kikao hicho
Balozi wa Kuwait Nchini, Mubarak Mohamed Alsehaijan alisema Tanzania ni
nchi salama na wameamua kubadilishana uzoefu katika usimamiaji na
udhibiti wa mipaka.
“Tuna uhusiano mzuri baina ya
Kuwait na Tanzania,tumekubaliana kubadilisha uzoefu ili kuweza
kuimarisha sekta ya ulinzi kwa kutumia teknolojia itakayorahisisha
udhibiti wa mipaka hapa nchini Tanzania” alisema Balozi Mubarak
Katika mazungumzo hayo pia
walijadili juu ya teknolojia ya udhibiti wa majanga ikiwemo moto na
ajali ambapo pia ni eneo ambalo nchi hizo mbili zilishaanza kushirikiana
katika shughuli za uokozi.
No comments:
Post a Comment