Timu
ya wataalamu wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) kwa kushirikiana na
Mkandarasi ABB wa nchini Switzerland, wameendelea na kazi ya kufunga
transfoma yenye uwezo wa Megawati 240 katika Kituo Kikuu cha Kupoza na
Kusambaza umeme cha Ubungo jijini Dar es Salaam.
Kwa
mujibu wa taarifa ya TANESCO iliyoitoa leo imesema transfoma hiyo
iliingia hapa nchini Januari 28, 2019 na lengo ni kuendelea kuboresha
hali ya upatikanaji wa umeme wa uhakika na kuleta ufanisi katika
usambazaji wa umeme katika jiji la Dar es Salaam na Pwani.
Akielezea uwezo wa Transfoma hiyo, Mkuu wa Kituo cha Kupoza na Kusambaza umeme Ubungo, Mhandisi Joseph Msumali amesema transfoma hiyo yenye uwezo wa kusukuma takribani Megawati 240 kutoka kwenye msongo wa kilovoti 220 kuelekea Msongo wa kilovoti 132 kwa ajili ya usambazaji na matumizi ya nishati ya umeme katika Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

Ufungaji wa Transfoma ukiendelea
No comments:
Post a Comment