Na Veronica Simba – Entebbe
Kamishan
wa Umeme na Nishati Mbadala, Mhandisi Innocent Luoga, kutoka Wizara ya
Nishati, ameongoza timu ya wataalamu wa nishati kutoka Tanzania,
kushiriki katika mkutano wa 26 wa Kamati Tendaji unaojadili mifumo ya
kusafirisha umeme, iliyounganishwa katika nchi zilizopo Mashariki mwa
Afrika (Eastern Africa Power Pool – EAPP)
Mkutano
huo unaofanyika leo, Februari 20, katika mji wa Entebbe nchini Uganda,
ni wa ngazi ya wataalamu kutoka nchi wanachama, ukiwa ni utangulizi wa
mkutano wa 14 wa Baraza la Mawaziri wa sekta husika unaotarajiwa
kufanyika kesho, Februari 21, 2019.
Miongoni mwa masuala yanayojadiliwa, ni pamoja na maboresho ya mkataba wa ushirikiano kwa nchi wanachama wa EAPP. Aidha,
mkutano unajadili masuala ya biashara ya kuuziana na kusafirisha umeme
kupitia mifumo ya EAPP na SAPP (Southern Africa Power Pool). Nchi wanachama wa EAPP ni Tanzania, Uganda, Kenya, Ethiopia, Libya, Sudan, Misri, Rwanda, DRC na Djibouti.
Mbali
na Kamishna Luoga, wataalamu wengine wanaoshiriki mkutano huo kutoka
Tanzania ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO)
Dkt. Tito Mwinuka, Mhandisi Christopher Bitesigirwe kutoka Wizara ya
Nishati, Mhandisi Meksesius Kalinga kutoka TANESCO pamoja na Mhandisi
Pius Gaspar kutoka TANESCO.
Katika
mkutano wa 14 wa Baraza la Mawaziri hapo kesho, Naibu Waziri wa
Nishati, Subira Mgalu atamwakilisha Waziri wa Nishati, Dkt. Medard
Kalemani.
Timu
ya wataalamu wa nishati kutoka Tanzania, inayoshiriki katika mkutano
unaojadili kuhusu mifumo ya kusafirisha umeme iliyounganishwa katika
nchi za Mashariki mwa Afrika (Eastern Africa Power Pool – EAPP), mjini
Entebbe, Uganda. Kamishna wa Umeme na Nishati Mbadala, Mhandisi Innocent
Luoga (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka (wa
pili – kulia), Mhandisi Christopher Bitesigirwe kutoka Wizara ya
Nishati (kulia), Mhandisi Meksesius Kalinga kutoka TANESCO (kushoto)
pamoja na Mhandisi Pius Gaspar kutoka TANESCO (wa pili - kushoto).
Wataalamu
wa nishati kutoka nchi wanachama wa Eastern Africa Power Pool (EAPP),
wakiwa katika picha ya pamoja, kabla ya kuanza mkutano wao uliojadili
masuala mbalimbali kuhusu mifumo ya kusafirisha umeme iliyounganishwa
katika nchi husika. Mkutano huo umefanyika Februari 20, 2019 mjini
Entebbe, Uganda.
Kamishna
wa Umeme na Nishati Mbadala, Mhandisi Innocent Luoga, akiwa katika
mkutano wa 26 wa Kamati Tendaji unaojadili mifumo ya kusafirisha umeme,
iliyounganishwa katika nchi zilizopo Mashariki mwa Afrika (Eastern
Africa Power Pool – EAPP)
Mkurugenzi
Mtendaji wa TANESCO, Dkt. Tito Mwinuka (wa kwanza – kulia), akiwa
katika mkutano wa 26 wa Kamati Tendaji unaojadili mifumo ya kusafirisha
umeme, iliyounganishwa katika nchi zilizopo Mashariki mwa Afrika
(Eastern Africa Power Pool – EAPP).
Mhandisi
Christopher Bitesigirwe kutoka Wizara ya Nishati (kushoto) na Mhandisi
Meksesius Kalinga kutoka TANESCO (kulia), wakiwa katika mkutano wa 26 wa
Kamati Tendaji unaojadili mifumo ya kusafirisha umeme, iliyounganishwa
katika nchi zilizopo Mashariki mwa Afrika (Eastern Africa Power Pool –
EAPP).
No comments:
Post a Comment