Na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula
ameagiza kuanza mchakato wa kuwaorodhesha watumishi wa umma ambao
hawajalipa kodi ya pango la ardhi hadi sasa ili wafikishwe katika
Mabaraza ya Ardhi na Nyumba.
Dkt.
Mabula ameyasema hayo alipofanya ziara katika Wilaya ya Bunda na
Serengeti mkoani Mara na wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza wakati wa ziara
yake inayoendelea ya kuhamasisha malipo ya kodi ya pango la ardhi
katika kanda ya ziwa.
“Nyinyi
watumishi wa Serikali mnatakiwa kuwa wa mfano katika kulipa kodi za
serikali kwa sababu hatuwezi kwenda kudai wengine wakati sisi wenyewe
hatujalipa kodi ya pango la ardhi, na kokote ntakapopita nataka majina
ya watumishi ambao hawajalipa ili wafikishwe katika mabaraza”
alisisitiza Dkt. Mabula.
“Mheshimiwa
Rais anasimamia miradi mikubwa hapa nchini kama ule wa ujenzi wa Reli
ya kisasa (SGR), ujenzi wa bwawa la kufua umeme wa Mto Rufiji,
Stiegler's Gorge na uimarishaji wa Shirika la Ndege la Tanzania ambayo
miradi hii yote inategemea kodi na mapato ya ndani, hivyo ni lazima
tumuunge mkono katika kulipa kodi hizi” aliongeza Dkt. Mabula.
Wakati
akiwa Wilayani Ukerewe alipokea taarifa ya afisa ardhi wa Halmashauri
ya wilaya hiyo Tewe Shaban kuwa hadi sasa halmashauri yake imeshakusanya
jumla ya Tsh 41,288,175 wakati lengo ni 100,000,000 kwa mwaka wa fedha
2018/2019, ambayo ni sawa na 41.2% iliyokusanywa.
Afisa
huyo alimueleza Dkt. Mabula kuwa hadi sasa jumla ya ilani 131 zenye
thamani ya Tshs 54,446,550 za madai ya kodi ya ardhi zimesambazwa kwa
wadaiwa kodi ya ardhi ambao wameanza kupunguza madeni yao na mpaka sasa
wameshalipa Tshs. 3,100,700 na kubaki Tshs. 51,345,850.
Baada
ya kupokea taarifa hiyo Dkt. Mabula alishangazwa na ukusanyaji huo
hafifu wa maduhuli ya Serikali na alimuagiza Afisa huyo kuwafikisha
mahakamani wadaiwa sugu wa kodi ndani ya mwezi mmoja kuanzia leo, na
aanze na watumishi wote wa Serikali katika halmashauri ya wilaya ya
Ukerewe.
Katika
kuhakikisha linatekelezwa hilo Dkt. Mabula akaagiza kuwepo kwa
Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi atakayesimamia kesi hizo na kuzitolea
hukumu kwa wadaiwa sugu waweze kulipa kwa wakati na kama hawatotekeleza
basi milki zao zitauzwa ili kulipwa deni hilo.
Akiwa
wilayani Bunda Dkt. Mabula alimuagiza afisa ardhi mteule kumfikishia
majina ya maafisa wa halmashauri ya wilaya ya Bunda ambao wanadaiwa kodi
ya pango la ardhi na hawajalipa hadi sasa wakati muda wa kulipa kwa
hiari ushaisha tangu tarehe 31 januari 2018.
Vivyohivyo
Dkt. Mabula akiwa katika Halmashauri ya wilaya ya Serengeti amamuagiza
Afisa Ardhi Mteule kukabidhi majina ya watumishi wa umma ambao wadaiwa
wa kodi ya ardhi kwa mkurugenzi wa halmashauri hiyo ili waweze
kufikishwa katika baraza ardhi iwapo watakuwa hawajalipa.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula
akimuagiza Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ukerewe Tewe Shaban
kuwa na usimamizi mzuri wa makusanyo ya Kodi ya pango la ardhi na kuwa
mfumo mzuri wa uhifadhi wa nyaraka za ardhi.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula
akiongea na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe
mkoani Mwanza.
Baadhi
ya watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza
wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt.
Angeline Mabula wakati alipofanya ziara katika wilaya hiyo. Picha zote
Na. Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi.
Naibu
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angeline Mabula
akimuagiza Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ukerewe Tewe Shaban
kuwa na usimamizi mzuri wa makusanyo ya Kodi ya pango la ardhi na kuwa
mfumo mzuri wa uhifadhi wa nyaraka za ardhi. Picha zote na Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi.
No comments:
Post a Comment