Pia, Waziri Mkuu amewataka watendaji wa
halmashauri hiyo kumaliza haraka migogoro yao ya kiutendaji kabla ya
Serikali haijawachukulia hatua kwani wanachokifanya ni kinyume na
maelekezo yake.
Waziri Mkuu
amechukua hatua hiyo leo (Jumanne, Februari 19, 2019) wakati akizungumza
na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo kwenye ukumbi wa
halmashauri hiyo akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Kigoma.
“Katika Serikali hii suala la ukusanyaji
wa mapato ni jambo nyeti na limepewa kipaumbele, hivyo ni lazima fedha
inayokusanywa itumike kama ilivyokusudiwa ikiwa ni pamoja na uboreshaji
wa miradi ya maendeleo kwa wananchi.”
Waziri Mkuu amesema wananchi wa
halmashauri hiyo wanalipa kodi kupitia kwa watendaji wa kata katika
maeneo yao lakini Mweka Hazina haingizi kwenye mfumo wa Serikali.
“Jambo hili halivumiliki.”
Amesema mbali na fedha za makusanyo ya
kodi pia matumizi ya fedha mbalimbali zinazopelekwa na Serikali katika
halmashauri hiyo nayo hayaridhizishi. Ametoa mfano wa fedha za sekta ya
Afya ambapo zaidi ya bilioni mbili zimepelekwa na dawa hakuna.
Waziri Mkuu amesema uaminifu na uadilifu
ni jambo ambalo linapaswa kupewa kipaumbele na watumishi wa umma, hivyo
amewataka watumishi hao wasijiingize kwenye mambo ambayo hayana tija
katika utumishi wao.
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema Serikali
imewapa dhamana watumishi hao kwa ajili ya kuwatumikia wananchi na si
kutanguliza maslahi yao binafsi, amewataka wajirekebishe kwa kutekeleza
majukumu yao ipasavyo.
“Serikali haitawapa nafasi ya kuendeleza
migogoro yenu kila mmoja lazima atambue majukumu yake na kuyatekeleza.
Serikali haiitaji mtumishi mvivu, masiyekuwa muadilifu na wala
anayejihusisha na vitendo vya rushwa.”
Amesema ni lazima wakamaliza migogoro ya
kiutendaji ambayo imesababisha watendaji wa halmashauri kutoelewana na
kugawanyika katika makundi na kushindwa kutekeleza majukumu yao
ipasavyo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, FEBRUARI 19, 2019.
No comments:
Post a Comment