Waandishi
kutoka vyombo mbalimbali vya habari nchini Tanzania, wakimsikiliza
Ofisa Mtendaji Mkuu wa African Wildlife Foundation Kaddu Sebunya
(kushoto).
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa African Wildlife Foundation Kaddu Sebunya akizungumza
leo jijini Dar es Salaam kuhusu umuhimu wa nchi za Afrika kuweka
mikakati itakayosaidia kulinda uhifadhi wa mazingira na wanyamapori.
*Yapongeza juhudi za Serikali katika kukomesha ujangili
*Yazishauri nchi za Afrika kulinda na kuhifadhi wanyamapori
African
Wildlife Foundation imesema Tanzania ndio nchi inayoongoza kwa kuwa na
Simba wengi na kwa upande wa Tembo inashika nafasi ya tatu barani
Afrika.
Imesema
hiyo inatoka na juhudi ambazo zinafanywa na Serikali ya Tanzania
kuhakikisha wanyamapori na uhifadhi wa misitu unapewa kipaumbele.
Hayo
yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Ofisa Mtendaji Mkuu wa African
Wildlife Foundation Kaddu Sebunya wakati akizungmzia umuhimu wa
uhifadhi wa wanyamapori na uhifadhi wa mazingira kwa nchi za Bara la
Afrika.
"Serikali
ya Tanzania ni mfano wa kuigwa katika eneo hilo la uhifadhi wa misitu
na utunzaji wa wanyamapori. Hii imefanya katika nchi za Bara la Afrika
,Tanzania kushika nafasi ya kwanza kwa kuwa na Simba wengi na na
inashika nafasi ya tatu kwa kuwa na tembo wengi. Nchi inayoongoza kwa
kuwa na tembo wengi ni Botswana ikifuatiwa na Zimbabwe,"amesema Sebunya.
Amesisitiza
ni muhimu wa kila nchi barani Afrika kuweka mikakati itakayosaidia
maliasili zilizopo kutunzwa na kulindwa vema huku akieleza kwa sasa kuna
changamoto ya wanyamapori wengi hasa Simba na Tembo kupungua.
"Ukweli
Simba na Tembo wameendelea kupungua barani Afrika na sababu yake ni
uwepo wa majangiri na uwindaji haramu.Hivyo African Wildlife Foundation
tunahamasisha kila nchi kuweka mipango ambayo itasaidia kuwafanya Simba
na Tembo waendelee kuwepo,"amesema.
Amesema
kila nchi ikiamua hakuna ambacho kitashindikana ambapo ametoa mfano kwa
Serikali ya Awamu ya Tano namna ilivyofanikiwa kudhibiti majangiri
ukilinganisha na miaka ya nyuma.
"Katika
hili la kulinda wanyamapori na uhifadhi kila nchi ikiamua
inaweza.Niitolee mfano Tanzania miaka ya nyuma Tembo walikuwa wanauliwa
sana lakini leo hii tembo hao hao wako salama kutokana na hatua ambazo
Serikali inachukua,"amesisitiza.
Sebunya
amesema watu wa Bara la Afrika wana maisha yao na tamaduni zao ambazo
kimsingi zilizingatia uhifadhi wa misitu, mapori na wanyama lakini kadri
siku zinavyokwenda na kuingia kwa tamaduni za nchi nyingine
kumesababisha kuibuka kwa changamoto ambazo iko haja ya kuzikabili.
"Katika
nchi nyingi sana barani Afrika nusu ya wanyama walikuwa siku za nyuma
leo hawapo.Hivyo tutaendelea kuzihamasisha nchi za Afrika kuweka
kipaumbele katika eneo hilo.
"African
Wildlife tumekuwa tukifanya jitihada za kuhamasisha wadau kushiriki
kikamilifu katika uhifadhi wanyama.Ndio maana hata kile Chuo cha Mwika
ni sehemu ya mchango wetu. Watalaamu wengi uhifadhi wa mazingira ,
misitu na wanyamapori waliopo barani Afrika wamepikwa katika chuo
hicho,"amesema Sebunya.
Wakati huo huo Sebunya amesema kadri nchi zinapofanya maendeleo ni vema pia zikazingatia utunzaji wa mazingira."Nchi
za Afrika zinahitaji kuwa na maendeleo na wakati huo huo zinapaswa
kulinda mazingira.Ni mambo mawili yanayokwenda kwa pamoja,"amesema
Sebunya. Na Said Mwishehe
No comments:
Post a Comment