Matokeo chanyA+ online




Friday, March 8, 2019

IDADI YA WATUMIA INTERNET YAONGEZEKA KUFIKIA WATU MILIONI 23


NAIBU WAZIRI
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Atashasta Nditiye,akizungumza wakati wa kufungua kikao kazi cha wadau wa  TEHAMA kutoka sekta ya Umma,Binafsi na Taasisi za Elimu ya Juu wa Ufundi kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa ndaki ya TEHAMA Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
KAIMU
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Dkt.Jim Yonazi akitoa taarifa wakati wa ufunguzi wa  kikao kazi cha wadau wa TEHAMA kutoka Sekta ya ya Umma,Binafsi na Taasisi za Elimu ya Juu wa Ufundi kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa ndaki ya TEHAMA kilichopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
SEKTA
Mwakilishi kutoka  sekta binafsi Bw.Mugeta Mujungu akitoa taarifa katika kikao kikao kazi cha wadau wa TEHAMA kutoka Sekta ya ya Umma,Binafsi na Taasisi za Elimu ya Juu wa Ufundi kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa ndaki ya TEHAMA kilichopo Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
TEHAMA WADAU TEHAMAWADAU
Baadhi ya wadau kutoka sekta mbalimbali wakifuatlia mada zilizokuwa zikitolewa katika  kikao kazi cha wadau wa  TEHAMA kutoka sekta ya Umma,Binafsi na Taasisi za Elimu ya Juu wa Ufundi kilichofanyika leo kwenye ukumbi wa ndaki ya TEHAMA Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM)
AA A
Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Atashasta Nditiye akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa TEHAMA kutoka Sekta binafsi,Taasisi za Utafiti na Elimu ya Juu na Ufundi.


Serikali  imesema kuwa idadi ya watumiaji wa Internent imeongezeka kutoka 520,000 mwaka 2009 na kufikia zaidi ya watu milioni 23 kwa mwaka 2018 hii ni kutokana na jitahidi za  wadau mbalimbali katika sekta ya tehama.
Hayo yamebainishwa leo jijini Dodoma  na Naibu Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Atashasta Nditiye wakati akifungua  kikao cha wadau wa Tehama kutoka sekta binafsi,taasisi za utafiti na elimu ya juu na ufundi amesema kuwa juhudi za Serikali zimepelekea kuongezeka kwa watumaji wa internent kutoka 520,000 kwa mwaka 2009 hadi kufikia zaidi ya watu milioni 23 kwa mwaka 2018.
Naibu Waziri amesema kuwa  watumaaji hao ni zaidi ya lengo walilojiwekea la kufikia watumiaji milioni  20 ifikapo mwaka  2020.
Aidha amesema kuwa katika kutekeleza sera ya Taifa ya tehama Serikali imeendelea kutekeleza program mbalimbali pamoja na ujenzi wa mkongo wa Taifa,ujenzi wa kituo cha kimataifa cha kukusanya data,pamoja na kuanzisha huduma za seriakli mitandao.
Nditiye amesema kuwa  Serikali inatambua jitihada zinazofanywa na sekta binafsi katika kukuza mawasiliano ikiwemo ujezni wa mkongo wa taifa ambao umeongeza mchango katika pato la taifa.
Hata hivyo amesema kuwa mkongo huo uliojengwa nchini wenye zaidi ya kilomita 26,000, Serikali pekee imejenga kilomita 7560 ambapo kilomita zingine zimejengwa kwa mchango wa sekta binafsi.
Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano,Dk Jimmy Yonazi amesema lengo la mkutano huo ni kushirikiana katika kuelewa sera ya tehama inachangiaje katika uchumi wa viwanda.
“Kutambua na kushirikiana na sekta binafsi,kupokea maoni ya wadau ili kubaini maeneo ya kufanya marejeo na kutafuta utaratibu wa kushirikiana kati ya serikali na sekta binafsi,”amesema Dkt. Yonazi.
Naye Mwakilishi wa sekta binafsi,Mugeta Mujungu amesema kuwa changamoto kubwa wanayokutana nayo ni sekta binafsi kutoshirikishwa wakati wa uandaaji wa sera mbalimbali.Picha na Alex Sonna-Fullshangweblog

No comments:

Post a Comment