Na Tiganya Vincent
U0ngozi
wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora(UYUI) umeagizwa kuongeza kasi katika
ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ili ifikapo Juni mwishoni mwaka huu
majengo yote waliyopangiwa yamewe yamekamilika.
Agizo
hilo limetolewa leo wilayani Uyui na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani Jafo baada ya kukagua
maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo na kutoridhishwa na kasi
ya ujenzi huo.
Alisema fedha zipo hakuna sababu ya kazi ya ujenzi kwenda pole pole kwa kuwa wananchi wanasubiri huduma hiyo kwa hamu.
Jafo
alisema katika Halmashauri nyingine ambapo walipewa fedha pamoja tayari
majengo yao yako usawa wa madirisha lakini ya Uyui bado yako katika
ngazi za msingi.
Alisema
sio vizuri kutumia fundi mmoja kujenga majengo yote ni vema wakatumia
mafundi wengi ili kuharakisha kazi ya ujenzi wa Hospitali hiyo.
Aidha
Waziri huyo alisema ni jambo la kusikitishwa kuona Halmashauri hiyo
imetumia kiasi cha milioni 8 kusafisha eneo badala ya kuwahamisha
wananchi kushiriki katika usafishaji wa ili fedha hizo zisaidie ujenzi.
Alisema
fedha walizozitumia katika usafishaji wa eneo zingeweza kusaidia katika
uendeleza wa ujenzi wa majengo hayo kama wananchi wangeshiriki katika
usafishaji wa eneo badala ya kukodi Greda na kulipa kiasi hicho cha
fedha.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya alimwakikishia Waziri kuwa
watajitahidi kukamilisha majengo hayo katika kipindi kilichopangwa na
kwa kuzingatia maelekezo ya TAMISEMI ili fedha zitakazobaki zisaidie
kujenga kichoma taka.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani
Jafo (kulia) akisalimiana na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya
Tabora -Uyui Said Ntahondi huku akishuhudiwa na viongozi mbalimbali
wakati wa ziara yake kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya
hiyo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani
Jafo (katikati) akiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Uyui Gift Msuya ( wa
pili kutoka kulia) kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya
hiyo.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani
Jafo (katikati) akitoa maagizo kwa viongozi wa Wilaya ya Uyui na wa
Hamashauri ya Wilaya ya Tabora -Uyui baada ya kukagua maendeleo ya
ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Selemani
Jafo (mbele) akiwaongoza viongozi wa Wilaya ya Uyui na wa Halmashauri ya
Wilaya ya Tabora -Uyui kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali ya
Wilaya hiyo. Picha na Tiganya Vincent
No comments:
Post a Comment