Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko akionyesha kwa kuuliza mwisho wa mpaka wa eneo la ujenzi wa TSF mpya, kushoto kwake ni Mkuu wa Wilaya Tarime.
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko
wa tatu kulia akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa Mara
wakielekea kwenye eneo la uchimbaji wa TSF kulia kwake ni mkuu wa mkoa
wa Mara, Adam Kigoma Malima.
Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko
wa kwanza kulia akimsikiliza mwenyekiiti wa kamati ya ulinzi na usalama
na mkuu wa mkoa wa Mara Adam Malima wa kwanza kushoto akitoa taarifa
fupi ya hali ya mkoa wake wakiwa kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya
Tarime.
Serikali imesema itaufunga mgodi
wa North Mara ifikapo Machi 30, 2019 endapo mgodi huo utashindwa
kuyadhibiti maji yenye sumu yanayo tiririka kutoka kwenye mabwawa ya
kuhifadhia maji (topesumu) (Tailings Storage Facility -TSF).
ya mgodi huo kuelekea kwenye makazi ya watu.
Hayo yamesemwa leo machi 5, 2019
na Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko alipotembelea mgodini hapo kwa
ziara ya kikazi ambapo pamoja na mambo mengine alitembelea mabwawa wa
topesumu (TSF) na kuzungumza na uongozi wa mgodi na baadae na wananchi
kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Nyamongo wilaya
ya Tarime kuzungumzia hatima ya malipo ya fidia za wananchi
waliohamishwa kupisha shuguli za mgodi.
Biteko amesema serikali
hairidhishwi na namna mgodi wa North Mara kwa jinsi wanavyo zingatia
swala la utunzaji wa maji yenye sumu kwenye (TSF) zao. Amesema serikali
inathamini sana maisha ya watu na mtu mmoja mmoja, na kwamba maisha ya
mtu mmoja ni bora kuliko shuguli zote za mgodi.
“ Naomba niseme ukweli, tena
kutoka moyoni, sijaridhishwa na hili jambo la utiririshaji wa maji yenye
sumu kuelekea kwenye makazi ya watu. Serikali hii ya awamu ya tano ya
Dkt. John Pombe Magufuli inathamini sana maisha ya watu wake kuliko kitu
chochote. Thamani yamaisha ya mtanzania mmoja ni bora kuliko
kinachochibwa hapa. Nitoe rai kwa mgodi ifikapo Machi 30, mwaka huu,
hili jambo liwe limekwisha, kinyume cha hapo, nitafunga mgodi mpaka pale
mtakapo tekeleza jambo hili” alisema Biteko.
Kwa upande wa uongozi wa mgodi
umesema, utatekeleza agizo hilo na kwamba juhudi za kudhibiti topesumu
kuelekea kwenye makazi ya watu limepewa kipaumbele na kwamba ndani ya
muda huo litakuwa limekamilika.
Katika ziara hiyo, Waziri Biteko
aliambatana na baadhi ya Maafisa wa Wizara hiyo akiwemo Kamishna wa
Madini Mha. David Mlabwa na Afisa Madini mkoa wa Mara Mha. Nyaisara
Mgaya, wengine ni kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa mara wakiongwa na
mwenyekiti wake ambae pia ni mkuu wa mkoa wa Mara bwana Adam Kigoma
Malima.
Ziara hiyo inafuatia vikao
mbalimbali vya awali vilivyofanyika mwaka huu vikilenga masuala
mbalimbali yanoyo husu mgodi huo likiwemo swala la udhibiti wa maji
yenye sumu (topesumu) yanayo lalamikiwa na wananchi wanaoishi kuzunguka
mgodi huo, kikao cha kwanza kilifanyika Januari 19, chini ya makatibu
wakuu wa wizara saba ((Madini, Makamu wa Rais Mazingira (NEMC), Ardhi,
TAMISEMI, Afya, Fedha na Maji)) ambapo serikali ilitoa miezi nane
kutekeleza maagizo yaliyopewa.
No comments:
Post a Comment