Waziri
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akivuta pazi pamoja na
mwenyekiti wa kampuni ya Cassava Starch of Tanzania Corporation, Gerald
Billet kuashiria ufunguzi wa kiwanda cha unga wa muhogo cha CSTC katika
kijiji cha mbalala mkoani Lindi.
Waziri
Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa akikata utepe ikiwa ni ishara ya
kufungua kiwanda cha kampuni ya Cassava Starch of Tanzania Corporation
(CSTC) cha unga wa muhogo wenye kiwango cha juu katika kijiji cha
mbalala, kata ya Nyegedi, mkoani Lindi. Wengine kutoka kulia ni Mhe.
Omary Mgumba (MB), naibu waziri wizara ya kilimo, mkuu wa wilaya ya
Lindi, Mhe. Shaibu Ndemanga, mwenyekiti wa kampuni ya CSTC bwana Gerald
Billet, Balozi wa ufaransa nchini Tanzania, Mhe. Frederic Clavier,
Mkurugenzi mtendaji wa CSTC bwana Christophe Gallean na mbunge wa jimbo
la Mtama mkoani Lindi, Mhe. Nape Nnauye.
Waziri
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (MB) kiwasha mashine ya mihogo
wakati wa ufunguzi wa kiwanda cha unga wa muhogo cha kampuni ya CSTC
mkoani Lindi.
Waziri
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (MB) kipewa maelezo kuhusu
taratibu za kiwanda cha unga wa muhogo baada ya kukifunguwa rasmi katika
kijiji cha Mbalala, mkoani Lindi.
Waziri
Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (MB) akiangalia mihogo
inavyopita kwenye mashine wakati wa ufunguzi wa kiwanda cha unga wa
muhogo cha kampuni ya CSTC mkoani Lindi.
Kiwanda cha kisasa cha kuzalisha unga
wa muhogo wenye kiwango cha juu cha kampuni ya ulimaji na usindikaji
muhogo ya Tanzania ijulikanayo kama Cassava Starch of Tanzania
Corporation – CSTC kimefunguliwa rasmi na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim
Majaliwa Majaliwa (MB) pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo
Christophe Galléan.
Kiwanda hicho ambacho ni cha aina ya
kipekee katika soko la Tanzania kina uwezo wa kuzalisha zaidi ya tani 1
ya unga wa Muhogo wenye kiwango cha juu ndani ya saa moja na kadiri ya
tani 6,000 kwa mwaka.
Akifunguwa kiwanda hicho Waziri Mkuu
alitoa pongezi kwa kampuni hiyo kwa kuchangia juhudi za serikali katika
kuinua uchumi kupitia viwanda. Aliipongeza kampuni hiyo kwa uwekezaji
mkubwa waliotekeleza katika mkoa wa Lindi kwa kujenga kiwanda hicho cha
kisasa ambacho kitaendeleza kilimo cha muhogo na pia kutoa ajira kwa
wakazi wa mkoa huo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa CSTC,
Christophe Galléan alisema "Tunafurahi kuanzisha rasmi kiwanda cha
kwanza cha ubora wa hali ya juu na cha kisasa nchini Tanzania.
Tunajivunia sana uwepo wa kiwanda hiki na taswira inayoipa kampuni yetu
ya CSTC, mkoa wa Lindi na Tanzania kwa ujumla. Tunashukuru sana kwa
ushirikiano wa serikali chini ya uongozi wa Rais John Magufuli, na
utekelezaji wako Waziri Mkuu Kassim Majaliwa. "
Cassava Starch of Tanzania Corporation
iilianzishwa miaka saba iliyopita ikiwa na makao yake makuu mkoani Lindi
ikiwa na lengo kuu la kuuza ndani na nje ya nchi unga wa muhogo wenye
ubora wa hali ya juu kabisa. Kiwanda hicho ambacho kipo kimkakati karibu
na bandari ya Mtwara kitakuwa na uwezo wa kusafirisha bidha zake katika
masoko muhimu duniani yakiwemo ya Afrika ya Mashariki na Kusini,
Mashariki ya Kati, Marekani na Ulaya.
Mfumo wa utendaji wa CSTC ni kukuza
mazao yenye ubora wa hali ya juu katika mashamba makubwa yenye ufanisi
na kusimamiwa na CSTC. Vilevile kusindika mazao yote katika kiwanda
kilichopo eneo la karibu, Mfumo huu wa utendaji unaofuatwa na CSTC wa
kuzalisha mazao na kuwa na kiwanda cha usindikaji ni wa kipekee katika
soko la unga wa muhogo la Afrika.
CSTC ilianza kufanya kazi mwaka 2012
nchini ikiwa na wafanyakazi zaidi ya 400 ambao kati yao asilimia 97 ni
Watanzania. "Tunaendelea kuongeza wafanyakazi, kutoa mafunzo na
kuendelea kutoa fursa kwa vijana wengi za uongozi katika ngazi zote za
uendeshaji kuanzia kiwandani, mashambani na katika shughuli za utawala"
alisema Mr Galléan.
Kampuni ya CSTC ina mpango wa kujenga
kiwanda cha kusindika wanga kutoka kwenye muhogo katika siku za usoni na
kiwanda hicho kitategemea kutoa ajira zaidi kwa Watanzania. Mipango hii
itanufaisha jamii kwa ajira, miundo mbinu na huduma za kijamii ambazo
zinaendelea kutolewa katika vijiji mbali mbali mkoani Lindi. Kwa
kuanzia, CSTC imewekeza katika elimu kwa kujenga darasa la shule ya
msingi,ujenzi wa barababara na kukarabati miundombinu ya maji katika
kijiji cha Lipome.
Hapo baadaye, CSTC itaanzisha mpango wa
wakulima wadogo ambao utahusisha utoaji mafunzo kwa wakulima ili
wajifunze njia mpya na za kisasa za kilimo, kuanzia maandalizi sahihi ya
ardhi kwa ajili ya kuweza kuzalisha mazao bora na kuongeza mavuno ya
mazao yao. Lengo la programu hii pia ni kuwawezesha wakulima wadogo
kuweza kuzalisha mazao kwa gharama nafuu na hivyo kuongeza ushindani wao
katika soko la muhogo.
"Inashurtisha katika usindikaji wa
mazao kufanyika ndani ya masaa 24 baada ya mavuno. CSTC inaanzisha
mpango huo wa kutoa mafunzo ya kilimo kwasababu miundombinu katika
mavuno ni muhimu sana. Tunatafuta washirika ambao tutatekeleza nao mradi
huu na kuweka malengo sahihi ili kuweza kufaidisha sekta ya kilimo
katika kanda hii,” alisisitiza Mkurugenzi Christophe Galléan.
Christophe Gallean pia alimalizia kwa
kuishukuru serikali kwa ushirikiano wake kwa CSTC na kueleza kuwa ana
shauku kubwa kuanza upanuzi wa viwanda na mashamba ya kampuni hiyo hapo
baadaye.
No comments:
Post a Comment