Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan leo
tarehe 26, Machi 2019 amekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya NBC Ndugu Theobald Maingu Sabi ofisini kwake Ikulu,
jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
huyo amefika ofisini kwa Makamu wa Rais kwa lengo la kujitambulisha
akiwa ameongozana na Meneja mahusiano na Serikali William Kalaghe pamoja
na Afisa Masoko wa NBC Bi. Neemarose Singo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Ndugu Theobald Maingu
Sabi (kushoto) ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC
Ndugu Theobald Maingu Sabi, Afisa Masoko wa NBC Bi. Neenarose Singo
pamoja na Meneja wa Mahusiano na Serikali Ndugu William Kallaghe (kulia)
mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake Ikulu, jijini Dar es
Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC
Ndugu Theobald Maingu Sabi (kushoto) mara baada ya mazungumzo ofisini
kwake Ikulu, jijini Dar es Salaam.
(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
No comments:
Post a Comment