Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
ametoa wito kwa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na wanawake kwa ujumla
kuchapa kazi zaidi na kushikamana katika kuleta maendeleo kwa jamii
nzima.
Makamu
wa Rais ameyasema hayo kwenye Kongamano la Wanawake la Kumpongeza
Mheshimiwa Dkt. Ali Mohammed Shein, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Baraza la Mapinduzi kwa kutekeleza ilani ya Uchaguzi ya Chama cha
Mapinduzi lililofanyika kwenye hoteli ya Verde, wilaya ya Magharibi A,
mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
“Sisi
ni sehemu muhimu sana ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha
Mapinduzi, hivyo Kongamano hili liwe chachu yetu katika kuchapa kazi
zaidi”alisema Makamu wa Rais.
Aidha,
aliwasihi wanawake kuchukua jukumu la kuzisemea na kuzitangaza kwa
sauti kubwa kazi nzuri zinazofanywa na viongozi wa Serikali zetu mbili
ili wananchi wazijue na wasipotoshwe.
“Sote
ni mashuhuda wa kazi kubwa na nzuri iliyofanyika hapa Zanzibar kwa
kipindi cha miaka mitatu. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya
Uongozi mahiri wa Dokta Shein imefanya kila liwezekanalo kuboresha hali
ya maisha ya wananchi wa Zanzibar kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo
katika sekta zote za kijamii, kisiasa na kiuchumi.”Alisisitiza Makamu
wa Rais.
Rais
Shein ametekeleza kwa umahiri mkubwa ilani ya Uchaguzi na kuweza kuleta
mafanikio makubwa katika Uimarishaji wa Huduma za afya, Elimu , ujenzi
wa miundombinu,Kilimo, ufugaji, uvuvi na Ushirika, kuwawezesha Wazee,
wanawake na Walemavu na kuwateua wanawake kwenye nafasi za Uongozi.
Makamu
wa Rais ameupongeza uongozi wa UWT Taifa pamoja na Ofisi ya Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar kwa kuandaa kongamano hilo ambalo sit u la
kumpongeza Dkt. Shein kwa kazi kubwa aliyofanya kwa kipindi cha miaka
mitatu, bali Kongamano la kutoa ushuhuda kwa wananchi kuhusu kazi nzuri
inayofanywa na Chama Cha Mapinduzi katika kusimamia maendeleo ya
wananchi.
Mawaziri
wa SMZ , Wawakilishi wa Viongozi na Naibu Waziri wa Nishati kutoka
Serikali ya Jamhuri ya Muungano walipata nafasi ya kuelezea mafanikio ya
utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM katika Kongamano hilo.
Kongamano
hili lilifanyika Pemba tarehe 9, Machi 2019 ambapo lilitanguliwa na
ziara liyoanza tarehe 6-8 mwezi Machi 2019 na ziara kama hiyo imefanyika
Unguja kuanzia tarehe 11-14 Machi 2019 ambapo tarehe 15 Kamati ya
Utekelezaji ya UWT Taifa ilikutana.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan
akihutubia kwenye Kongamano la UWT la kumpongeza Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein kwa utekelezaji
wa ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi lililofanyika kwenye hotel
ya Verde. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
No comments:
Post a Comment