Wajumbe
wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC) wakipokea
taarifa za maendeleo ya miradi ya gesi asilia jijini Dar es Salaam
wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba (mwenye overall
ya bluu) akiwaonyesha wajumbe wa Kamati ya Bunge ya PIC kazi ya
kusambaza gesi asilia kwa wateja kwa matumizi ya majumbani. Kushoto ni
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mhe. Dkt. Raphael Chegeni.
Mhandisi
Dora Ernest (alieshika mic ya TBC) akitoa maelezo ya huduma ya
kusambaza gesi asilia kwa matumizi ya nyumbani kwa wajumbe wa Kamati ya
Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma (PIC).
Kamati
ya Bunge inayosimamia uwekezaji wa mitaji ya umma (PIC) imefanya ziara
ya kikazi kukagua maendeleo ya miradi ya gesi asilia jijini Dar es
Salaam.
Kamati
hiyo inayoongozwa na Mhe. Dkt. Raphael Chengeni ilitembelea kituo cha
kupokea gesi asilia Kinyerezi na kujionea kazi za kitaalam zinazofanywa
na wazawa katika kupokea gesi na kuisambaza kwa wateja mbalimbali
wakiwemo wazalishaji umeme.
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Mhandisi Kapuulya Musomba akitoa wasilisho
juu ya mikakati ya TPDC katika kujiendesha kibiashara alisema “katika
mwaka huu wa fedha tunategemea kuanza kutoa gawio Serikalini”. Mhandisi
Musomba aliieleza Kamati ya PIC kwamba kwa sasa Shirika liko katika
mageuzi makubwa ya kiutendaji nia ikiwa ni kuongeza ufanisi na hatimaye
kutengeneza faida itakayoruhusu kutoa gawio kubwa Serikalini.
Katika
kipindi cha miaka mitatu TPDC imekuwa ikijeindesha kwa hasara kutokana
na uwekezaji mkubwa uliofanywa katika ujenzi wa miundombinu ya gesi
asilia.
Nae
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma, Mh. Dkt.
Raphael Chengeni alisema “Sisi kama Kamati tumefurahishwa sana na
mageuzi makubwa ambayo yanaendelea kufanyika TPDC kwani hili lilikuwa
moja ya Shirika ambalo linaonekana kuwa mzigo kwa Serikali kwa kushindwa
kutoa gawio kwa Serikali”.
Dk.
Chengeni aliongeza kwamba kwa taarifa waliyopokea TPDC sasa wanaamini
mambo yatakuwa mazuri katika Shirika hili ambalo linategemewa sana
katika kufikia Tanzania ya viwanda kwa kuzingatia upekee wa bidhaa
wanayozalisha, gesi asilia. Wajumbe wengine wa PIC pia walionekana
kuridhishwa na utekelezaji wa miradi na mageuzi ambayo TPDC imeshaanza
kuyafanya.
Katika
ziara hiyo Wabunge walipata nafasi ya kutembelea eneo la Ubungo na
kujionea wa mtambo wa kupunguza mgandamizo wa gesi kwa ajili ya
kusambaza kwa wateja wa majumbani na viwandani. Pia walitembelea maeneo
ya Mlimani City na kujionea zoezi la kuunganisha gesi kwa wateja wa
majumbani na baadae kiwanda cha Coca-Cola maeneo ya Mikocheni ambao nao
wanatarajiwa kuanza kutumia gesi baada ya kazi ya kuunganisha
kukamilika.
Kamati
ya Bunge ya Uwekezaji wa Mitaji ya Umma inaangalia mambo matatu
makubwa, kwanza gawio linalokwenda Serikalini, kupokea mtaji unaozidi na
suala la mapato ghafi ambayo ni 15%, alieleza Mwenyekiti wa Kamati, Dk.
Raphael Chegeni.
No comments:
Post a Comment