Wakala
wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi umepongezwa na Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Katiba na Sheria kwa kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa
weledi ili kusaidia nguvu kazi iliyopo kutumika kuchochea maendeleo.
Akizungumza
wakati wa semina kwa wabunge wa Kamati hiyo iliyofanyika Machi 27, 2019
katika Bungeni Dodoma, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe.Mohamed Mchengelwa
amesema kuwa Wakala huo umeonesha mfano bora katika kutekeleza
majukumu yake na pia kwa kuwajengea uwezo wabunge kuhusu masuala ya
usalama mahala pa kazi na umuhimu wake katika kutekeleza majukumu yao ya
kila siku.
“Elimu
tuliyopata ni muhimu kwetu na kwa wananchi hivyo pamoja na kazi nzuri
mnayofanya ni vyema sasa elimu hii ikatolewa kwa wananchi wote na
wabunge kwa ujumla ili kusaidia kupunguza athari zinazotokana na
kukosekana kwa elimu kuhusiana na masuala ya Usalama Mahali Pa Kazi
ikiwemo namna ya kutoa huduma ya kwanza,” alisisitiza Mchengelwa
Akifafanua
amesema kuwa katika masuala ambayo Kamati hiyo imetoa ni pamoja na
kuongeza kiwango cha utoaji wa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari.
Kwa
upande wake Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi,
Ajira na Vijana Mhe. Antony Mavunde amesema kuwa dhamira ya Serikali ni
kuhakikisha kuwa wabunge wanapata uelewa kuhusu utekelezaji wa majukumu
ya OSHA.
Aliongeza
kuwa kuna umuhimu mkubwa wakuwajengea uwezo wabunge kama wawakilishi wa
wananchi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
“Lengo
letu kama Serikali ni kuhakikisha kuwa tunalinda nguvu kazi iliyopo ili
iweze kusadia katika ujenzi wa uchumi wa viwanda na maendeleo ya Taifa
kwa ujumla,” alisisitiza Mavunde
Kwa
upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA Bi. Khadija Mwenda amesema kuwa
wameandaa semina hiyo kwa wabunge ili kuwajengea uwezo wa kujikinga na
athari za ajali au panapotokea mgonjwa anayehitaji kupata msaada wa
huduma ya kwanza katika mazingira yao ya kazi na mengine
yanayowazunguka.
Aliongezea
kuwa OSHA itaendelea kutoa elimu kwa umma ili kujua namna bora za
kujilinda na kujiepusha na madhara yanayoweza kuwapata wawapo kazini
pamoja na mazingira yote yanayowazunguka kwa kuzingatia misingi ya elimu
ya utoaji wa huduma ya kwanza endapo kunatokea dharula au majanga
kazini.
“Tumejipanga
kuwafikia watanzania kwa wingi wao ili kutoa elimu kwa umma juu ya
masuala ya Usalama mahala Pa Kazi kwa kuzingatia unyeti wa masuala hayo
kwani ni muhimu wananchi wakaelewa namna bora za kujilinda kuepuka
madhara wawapo kazini,”alisema Bi.Mwenda
OSHA
imekuwa ikiwajengea uwezo makundi mbalimbali katika jamii ikiwemo
wabunge na wananchi ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi na
kuilinda nguvu kazi iliyopo kwa maslahi mapana ya Taifa letu.
Kaimu
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Afya na Usalama Mahala Pa Kazi Bi. Khadija
Mwenda akieleza umuhimu wa kuzingatia kanuni za kutoa huduma ya kwanza
kwa mgonjwa au mtu aliyepata ajali wakati wa semina kwa wajumbe wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Machi 27, 2019 Jijini
Dodoma.
Mkurugenzi
wa Mafunzo na Tafiti na Takwimu kutoka Wakala wa Afya na Usalama mahala
pa Kazi (OSHA) Joshua Matiko akiwasilisha mada wakati wa semina ya
kuwajengea uwezo wabunge ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi
na kuongeza tija.
Mkurugenzi
wa Mafunzo na Tafiti na Takwimu kutoka Wakala wa Afya na Usalama mahala
pa Kazi (OSHA) Joshua Matiko akiwasilisha mada wakati wa semina ya
kuwajengea uwezo wabunge ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi
na kuongeza tija.
Sehemu
ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria
wakifuatilia semina ya kuwajengea uwezo kuhusu majukumu ya OSHA leo
jijini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria Mhe. Dkt. David Mathayo akichangia jambo wakati wa mafunzo hayo.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
No comments:
Post a Comment