Bodi
ya Utalii Tanzania(TTB), Ipo katika hatua za mwisho za Mazungumzo na
Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania na Klabu ya Genk iliyopo
nchini Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta kuwa Balozi wa kutangaza Utalii
wetu Kimataifa.
akziungumza
na Waandishi wa habari Mapema leo Jijini Dar es Salaam Mkurugenzi
Muendeshaji wa Bodi hiyo, Devotha Mdachi amesema kuwa katika hatua ya
kutangaza utalii kimataifa wameona wamtumie Mbwana Samatta.
"wote
tunajua umaharufu wa Mchezaji wetu katika ligi ya ubegiji na soka la
barani ulaya kwa sasa hivyo katika Malengo yetu ya kutumia watu maharufu
ambao ni Vijana wa kitanzania tumezungumza na Mbwana Samatta na
ametuambia kuwa ifikapo mwezi May atakapokuja katika mapumziko yake kila
kitu kitakamilika"anasema Mdachi.
ametaja
kuwa mbali ya Mbwana Samatta wapo wasanii wengi na Vijana Maharufu
ambao wanataraji kuwafikia hili wawe mabalozi wa utalii wetu nchini
lakini kwa kuanzia wameanza na Samatta pamoja na Miss Tanzania .
Samatta
atakuwa Kijana wa Pili wa Kitanzania Mwenye Mafanikio ambaye atapata
nafasi ya kuwa balozi wa TTB ambapo ametanguliwa na Miss Tanzania
2018/2019 Queen Elizabeth Mukune ambaye amesaini Mkataba leo.
No comments:
Post a Comment