Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba
J. Kabudi (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Mikhail Bogdanov,
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Shirikisho la Urusi katika Ofisi Ndogo
ya Wizara Jijini Dar es Salaam. Wamezungumzia masuala mbalimbali
yaliyolenga kuboresha na kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina ya
mataifa haya mawili, hususan, katika Nyanja ya kidiplomasia, nishati,
biashara na uwekezaji. Naibu Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi
ya siku mbili. Mawaziri
wanaendelea na mazungumzo hayo, huku ujumbe aliofuatana nao Naibu
Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi ukifuatilia mazungumzo hayo
utoka
kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Urusi, Mej. Jenerali mstaafu Simon
Mumwi, Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bw. Jestas
Nyamanga, Balozi wa Urusi nchini Tanzania, Mhe. Yuri Popov na Afisa wa
Ubalozi wa Urusi nchini Tanzania wakifuatilia mazungumzo ya Mawaziri.
No comments:
Post a Comment