Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James kulia akisaini
mkataba wa Mkopo wa Masharti nafuu wenye thamani ya Shilingi bilioni
589.26 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika AfDB iliyowakilishwa na
Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo hapa nchini Dkt. Alex Mubiru (kushoto
akisaini) katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Hazina jijini Dar es
Salaam. Fedha hizo zitatumika katika ujenzi wa barabara ya kiwango cha
lami kutoka Kabingo(Kakonko)-Kasulu-Manyovu km 260 mkoani Kigoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akibadilishana mkataba na
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) hapa nchini
Dkt. Alex Mubiru mara baada ya kutiliana saini mikataba miwili ya mkopo
wa masharti nafuu wa kiasi cha Shilingi bilioni 589.26 itakayotumika
katika ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka
Kabingo(Kakonko)-Kasulu-Manyovu km 260 mkoani Kigoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akionesha mkataba wa
mkopo wa masharti nafuu pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo
ya Afrika (AfDB) Dkt. Alex Mubiru mara baada ya kusaini katika Ofisi za
Hazina jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza jambo
kuhusiana na ramani ya ujenzi wa barabara ya kutoka
Kabingo(Kakonko)-Kasulu-Manyovu km 260 zitakazojengwa kwa kiwango cha
lami mkoani Kigoma.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza jambo na
wanahabari kuhusiana na mkopo huo wa masharti nafuu ambao utatumika
katika ujenzi wa barabara mkoani Kigoma. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara
ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya (Ujenzi) Arch. Elius
Mwakalinga.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza jambo
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya
(Ujenzi) Arch. Elius Mwakalinga
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Doto James akizungumza jambo na
Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Alex Mubiru
mara baada ya kusaini mikataba hiyo ya mkopo wenye masharti nafuu
katika Ofisi za Hazina jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment