Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe, akizungumza kwenye mkutano huo. Kulia ni Meneja Rasilimali za Shirika, Macrice Mbodo na kushoto ni Meneja Mkuu Uendeshaji Biashara wa TPC, Mwanaisha Ali Said.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Elia Madulesi, akizungumza wakati akimkaribisha Postamasta
Mkuu wa Shirika hilo, Hassan Mwang'ombe (kulia), kuzungumza na
waandishi wa habari kuelezea mkakati wa shirika katika kuimarisha maduka
yake ya kubadilishia fedha za kigeni nchini. Katikati ni Meneja Mkuu
Uendeshaji Biashara wa TPC, Mwanaisha Said.
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta wakiwa kwenye mkutano huo.
Baadhi ya Maofisa wa Shirika la Posta wakimsikiliza Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe, wakati akizungumza na waandishi leo jijini.
Postamasta Mkuu, Hassan Mwang'ombe (katikati), akuzungumza na waandishi wa habari kuelezea mkakati huo wa shirika.
Baadhi
ya wateja wakipata huduma kwenye maduka ya kubadilishia fedha za kigeni
ya Shirika la Posta leo, Ofisi ya Posta Kuu jijini Dar es Salaam.
Wateja wakiwa katika Kituo cha huduma mbalimbali za shirika wakisubiri kupatiwa huduma, Ofisi ya Posta Kuu jijini Dar es Salaam leo.
Moja ya maduka ya kubadilishia fedha za kigeni ya Shirika la Posta, jijini Dar es Salaam.
CHINI ni Taarifa iliyotolewa na Postamasta Mkuu kwa waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam leo
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU KUFUNGULIWA KWA MADUKA NA VITUO VYA KUBADILISHIA FEDHA ZA KIGENI VYA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA
Tarehe
28 february 2019 Benki kuu ya Tanzania ilitangaza kwamba maduka ya
kubadilishia fedha yatabaki kwenye mabenki, taasisi za kifedha pamoja na
maduka ya fedha za kigeni za Shirika la Posta Tanzania tu.
Tunapenda
kuutarifu umma wa watanzania kuwa Shirika la Posta limejizatiti katika
kutoa huduma hiyo kwa umma wa watanzania na tunapenda kuwajulisha kuwa
mpaka sasa tunavyo vituo kumi (10) vinavyotoa huduma ya kubadilisha
fedha ambapo ni Kariakoo, Posta Mpya, Kijitonyama, Oysterbay, City drive
(Sokoine ) , Libya Posta, Uwanja wa ndege, vituo hivi vyote vipo jijni
Dar es Salaam na mpaka ifikapo tarehe 15 Marchi 2019 tutakuwa na vituo
ishirini(20) vya kubadilishia fedha za kigeni.
Pia
tuna mikoa miwili ambayo tayari huduma hii imeanza nayo ni ofisi kuu ya
Posta Zanzibar na Arusha, Pia tunatarajia mwishoni mwa mwezi Marchi
mikoa 17 yenye ofisi za posta zitaanza kutoa huduma hiyo. Tungependa
kuutaarifu Umma ,watembelee katika vituo vyetu vya posta kupata huduma
hii ya ubadilishaji fedha za kigeni.
Shirika la Posta Tanzania linapenda kuujulisha Umma kupokea taarifa hii muhimu kwao na kwa maendelea ya Taifa.
imetolewa na ;
POSTAMASTA MKUU NA MTENDAJI MKUU
SHIRIKA LA POSTA TANZANIA
No comments:
Post a Comment