Waziri wa Elimu,Sayansi na
Teknolojiaa Profesa Joyce
Ndalichako anatarajiwa kuwa mgeni rasmi
katika mkutano wa kimataifa wa waratibu wa kitaifa wa miradi inayotekelezwa na
Shirika la nguvu za Atomiki duniani kwa nchi
46 kanda ya Afrika utakaofanyika kuanzia tarehe 11 hadi 15 mezi Machi jijini Arusha wenye lengo la kujadiliana na
masuala mbali.
Mkutano huo utashirikisha washiriki 60
kutoka nchini 46 duniani kutoka bara la Afrika ambao ni wanachama wa Shirika la nguvu za
Atomiki duniani ambao wataweza kujadiliana
masuala mbali mbali .
Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Nguvu za
Atomiki Tanzania ,Profesa Lazaro Busagala amaesema maandalizi ya mkutano huo
yamekamilika na kwamba wana imani mkutano huo utaweza kusaidia nchi washiriki
kuweza kusonga mbele katika namna ya uboreshaji wa sekta mbali mbali kutokana
na miradi inayofadhiliwa na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki
Duniani(IAEA).
Amesema katika mkutano huo ,washiriki
watapata nafasi ya kujadiliana kwa mapana juu ya namna ya.
Pia Profesa Busagala ameongeza kuwa
mkutano huo pia utahudhuriwa na
Mkurugenzi wa Shirika la Kimataifa
la Nguvu za Atomiki kanda ya AFrika Bwana Shaukat Abdrazak ambaye baada ya mkutano huo
ataweza kufanya mazungumzo na viongozi mbali mbali na uongozi wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar,Wizara nne ambazo zimekuwa zikihusika katika miradi mbali
mbali ya kitaifa inayotekelezwa na Shirika la Nguvu za Atomiki duninia(IAEA) .
Kwa upande wa Serikali ya
Mapinduzi Zanzibar ,Mkurugenzi Shaukat atakutana na Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo
na Uvuvi .
Kwa upande wa Tanzania Bara Shaukat
atafanya mazungumzo na Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na
Watoto, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano
wa Afrika Mashariki,Waziri wa Maji .
Pia ataweza kufanya ziara katika Taasisi
ya Utafiti wa Kilimo Seliani,Taasisi ya Chakula na Lishe na Taasisi ya Saratani
Ocean Road.
Profesa Busagala amesema kuwa mazungumo
hayo yataweza kusaidia nchi kwenye uboreshaji wa miradi mbali mbali
inayofanyika hapa nchini hasa katika sekta ya Afya,Kilimo,maji.
Ameeeleza kuwa Tanzania ni moja ya nchi
iiliyoweza kufadika kwa kiasi kikubwa kwa miradi katika ya udhibiti na kuhamasisha matumizi salama ya tekenolojia ya nyuklia
inayotekelezwa na Shirika la Nguvu za Atomiki duniani .
No comments:
Post a Comment