Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangala amewataka Watanzania
kuondokana na dhana iliyojengeka miongoni mwao kuwa watumishi wa Wizara
hiyo hususan wahifadhi wa wanyamapori na Misitu ni watu katili
wanaowatesa Wananchi.
Kauli
hiyo ameitoa leo wakati akifungua mkutano wa 26 wa Baraza la
Wafanyakazi wa Wizara hiyo uliofanyika katika Chuo cha Taaluma ya
Wanyamapori Pasiansi jijini Mwanza.
Amesema
watumishi hao ni watu wenye utu na weledi wa hali ya juu na
wanaozingatia sheria katika kutimiza majukumu yao na hulazimika kutumia
nguvu wakati wakipambana na majangili wanaokutwa katika maeneo ya
hifadhi wakifanya vitendo vya ujangili.
‘’
Ulinzi wa Rasilimali za nchi ni jukumu letu sote, wizara imepewa
dhamana ya kusimamia na kuongoza kwa niaba ya watanzania, kama kuna
watumishi wa Wizara hii wanaowanyanyasa wananchi naomba walete ushahidi
kwetu ili tuwachukulie hatua’’ amesema Dkt. Kigwangala.
Waziri
Kigwangala amesikitishwa na idadi ya watumishi walipoteza maisha kwa
ajali na wengine kuuwawa na majangili wakati wakipambana nao katika
maeneo yote ya hifadhi nchini na kutoa wito kwa wananchi wote wenye
taarifa au ushahidi juu ya vitendo vyovyote vya kihalifu kuziwasilisha
katika mamlaka zinazohusika.
Amesema
kuwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua wale wote wanaojihusisha na
vitendo vya ujangili na uhalifu katika maeneo ya hifadhi na wale wote
wanaoshirikiana na makundi ya watu wenye nia ovu ya kukwamisha juhudi za
uhifadhi wa rasilimali za Taifa.
Ametoa
wito kwa wananchi kuheshimu sheria za uhifadhi na kuepuka kuvamia
maeneo ya hifadhi kwa shughuli za kijamii na ufugaji akitoa wito kwa
viongozi mbalimbali wa Siasa kuunga mkono juhudi za wizara za ulinzi wa
maeneo ya hifadhi kwa kuwaelimisha wananchi wanaowaongoza kujiepusha na
vitendo vya uvamizi wa maeneo ya hifadhi badala ya kuwatetea.
Kwa
upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prof.Adolf
Mkenda akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao hicho amesema kuwa jumla
ya watumishi 23 walifariki dunia wakati wakitekeleza majukumu ya
uhifadhi na 5 walijeruhiwa na majangili wakiwa kazini.
Prof.
Mkenda amesema kuwa waliofanya vitendo hivyo hawaitakii mema Tanzania
na ni maadui wa shughuli za uhifadhi nchini akiongeza kuwa Serikali
itaendelea kusimama na kuwatetea watumishi na askari wa wanyamapori
wanaotimiza majukumu yao kwa kuzingatia sheria.
Katibu
Mkuu wa Maliasili na Utalii Prof, Adolf Mkenda akizungumza na
watumishi wa Wizara hiyo (hawapo Pichani) wakati wa ufunguzi wa baraza
la 26 la Wafanyakazi wa Wizara hiyo liliofanyika leo Jijini Mwanza.
Waziri
wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangala akisisitiza jambo wakati
akizungumza na Watumishi wa Wizara hiyo kuhusu umuhimu wa kutekeleza
maagizo kwa wakati yanayotolewa na Viongozi wa Wizara hiyo katika kikao
cha Baraza la 26 la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika leo
Jijini Mwanza.
Naibu
Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe,Constantine Kanyasu akizungumza na
Watumishj wa Wizara hiyo katika kikao cha Baraza la 26 la Wafanyakazi
kilichofanyika leo Jijini Mwanza.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla, Naibu Waziri wa
Wizara, Mhe, Constantine Kanyasu wakiwa wameshikana na watumishi
wengine hukuwakiimba wimbo wa mshikamano Daima katika Kikao cha Baraza
la 26 la Wafanyakazi kilichofanyika leo jijini Mwanza.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla akiwa ameambatana na
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Constantine Kanyasu wakati akikagua
gwaride la Jeshi Usu katika Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Pasiansi.
Wafanya
kazi wa Maliasili na Utalii wakiimba wimbo wa mshikamano Daima katika
Kikao cha Baraza la 26 la Wafanyakazi wa Wizara hiyo kilichofanyika leo
jijini Mwanza.
No comments:
Post a Comment