Ndoto ya Tanzania kuwa nchi ya uchuni wa kati ifikapo mwaka 2025 ipo karibu kutimia.
Hayo
yalisemwa jana na Dkt. Tausi Mbaga Kida, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi
ya Utafiti wa Masuala ya Uchumi na Jamii (Economic and Social Research
Foundation- ESRF) katika semina iliyoandaliwa kwa pamoja baina ya
taasisi hiyo na Benki ya Dunia kujadili safari ya Tanzania kuelekea
uchumi wa kati.
Akizungumza
katika semina hiyo, Dkt. Tausi Kida alisema kuwa hadi kufikia sasa pato
la wastani la mtanzania ni dola za kimarekani (USD) 910 wakati
inahitajika kwa taifa kufikisha kiwango cha pato la wastani la USD 995
kuwa taifa la uchumi wa kati.
“We
are almost there – tumekaribia kabisa kufika” Kinachotakiwa sasa ni
kuzidisha juhudi ili kasi ya ukuaji wa uchumi usishuke bali izidi
kuongezeka – alisema.
Ili
kuifikia lengo hilo, Dkt. Tausi Kida alishauri pia kufanyika mageuzi
katika sekta ya kilimo kwa kuongeza tija sambamba na kuongeza usindikaji
wa mazao ya kilimo hii ikiwa ni katika jitihada za kuondokana na kilimo
cha kujikimu na kujikita zaidi katika kilimo cha kibiashara chenye
kulenga mahitaji ya soko la ndani na nje.
Sambamba
na hilo, Dkt Tausi Kida alishauri pia kuongeza uwekezaji katika
rasilimali watu hususani kuboresha upatikaji wa huduma za afya, elimu na
maji kama njia ya uhakika ya kuondokana na umaskini ifikapo mwaka
2025.
Akifafanua
zaidi, Dkt Tausi Kida alieleza kwamba tangu mwaka 2000, Tanzania
imekuwa ikitekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa (Development Vision 2025)
inayolenga kuifikisha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo
mwaka 2025.
Dkt.
Tausi Kida aliwaeleza washiriki wa semina kuwa dira hiyo imelenga
kubadili uchumi wa Tanzania kutoka kutegemea sekta ya kilimo yenye tija
ndogo na kuwa taifa lenye kutegemea zaidi uchumi wa viwanda na hasa
viwanda vyenye kutengeneza bidhaa zenye ubora wa kumudu ushindani wa
soko la kimataifa.
Akifafanua
zaidi, Dkt Kida alisema kuwa Dira hii ya Maendeleo ya Taifa inalenga
pia kuondoa kabisa umaskini nchini Tanzania ifikapo mwaka 2025. “It is
envisioned that by 2025 abject poverty shall be something of the past –
ni ndoto yetu kwamba ifikapo mwaka 2025 suala la umaskini litakuwa ni
jambo lilipitwa na wakati nchini Tanzania” alisema.
Alieleza
kwamba Tanzania imekuwa ikitekeleza Dira ya Maendeleo ya Taifa kupitia
mikakati mbali mbali ikiwa ni pamoja na Mkakati wa Kwanza na wa Pili wa
Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini nchini Tanzania – mikakati ambayo
ilifahamika zaidi kwa jina la MKUKUTA na Mipango ya Miaka mitano mitano
ya Maendeleo ya Taifa ambapo kwa sasa taifa linatekeleza mpango wa pili
kwa kipindi cha miaka ya 2016/17 – 2020/21 alisema.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Benki ya Dunia kwa nchi za
Tanzania, Burundi, Malawi na Somalia Bi. Bella Bird alisema kwamba Benki
ya Dunia itaendelea kuimarisha ushirikiano wake na Tanzania uliojengeka
kwa zaidi ya miaka 54 sasa.
Ushirikiano
huu unalenga kuiwezesha Tanzania kuwa moja ya mataifa yenye uchumi
mkubwa duniani. Bi Bella aliuambia mkutano kwamba katika miaka hiyo
yote, Benki ya Dunia imekuwa ikitoa misaada ya kifedha kwa Tanzania hasa
kupitia Shirika lake la Kimataifa la Fedha (International Development
Association – IDA) ambalo limekuwa likitoa misaada katika nyanja mbali
mbali hususani afya, elimu, hifadhi ya jamii, maji, nishati, uchukuzi,
miji, mazingira, sekta za fedha na utawala bora.
Semina hiyo ilifanyika jana, Jumatano tarehe 21 mwezi wa 3 mwaka 2019 katika ukumbi wa mkutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Dhumuni
kuu ya semina hiyo lilikuwa ni kujadili safari ya Tanzania katika
kuekea uchumi wa kati. Semina hiyo ilichagizwa na mada iliyotolewa na
ndugu Yutaka Yoshino, mchumi mwandamizi wa Benki ya Dunia ambaye alitoa
mada juu ya uzoefu wa mataifa ya Vietnam na Bangladesh katika kufanya
mageuzi ya kiuchumi na maendeleo ya viwanda ambapo yamefanikiwa kupiga
hatua na kuwa mataiafa ya uchumi wa kati katika miaka ya hivi karibuni.
“Both
countries were at the same level of per capita income as Tanzania in
early 1990s - pato la wastani kwa mataifa haya lilikuwa sawa na lile la
Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 1990” alisema.
Baadhi
ya mataifa ya Afrika yaliyofanikiwa kutoka katika kundi la nchi maskini
zaidi duniani na kuwa mataifa yenye uchumi wa katika miaka ya hivi
karibuni ni pamoja na Ghana, Nigeria, Sudan na Zambia.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi
Kida (kulia) akisalimiana na baadhi ya washiriki kutoka Ubalozi wa
Ufaransa wakati wa semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na Taasisi ya
Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF)-juu ya safari ya Tanzania kuelekea
uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini
Dar es Salaam.
Ofisa
Mtendaji Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bi Bella Bird akiongozana na
mwenyeji wake Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na
Kijamii (ESRF), Dk Tausi Kida kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano mara
baada ya kuwasili kushiriki semina ya pamoja kati ya Benki hiyo na
Taasisi hiyo juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati
iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi
Kida akitoa neno la ukaribisho kwa washiriki (hawapo pichani) wakati wa
semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya
Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano
wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Ofisa
Mtendaji Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bi Bella Bird akitoa neno la
ufunguzi wa semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya
safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa
mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mchumi
wa Benki ya Dunia, Bw Yutaka Yoshino akitoa mada kuhusu safari ya
Tanzania kuelekea uchumi kati wakati wa semina ya pamoja kati ya Benki
ya Dunia na iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es
Salaam.
Dr
Jehovaness Aikaeli kutoka Idara ya Uchumi ya Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM) akielezea umuhimu wa umma na sekta binafsi kushirikiana
kutokana uhaba wa rasilimali wakati wa kujadili mada kwenye semina ya
pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea
uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini
Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mkazi wa TradeMark tawi la Tanzania, Bw John Ulanga (wa pili kushoto)
akizungumzia ukosefu wa masoko nchini Tanzania ambao unakwaza ukuaji wa
kilimo ambao ndio uti wa mgongo kwenye viwanda wakati wa kujadili mada
kwenye semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya
Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano
wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk Tausi
Kida (kulia) akizungumzia umuhimu wa kuangalia rasilimali watu kwa
kuzingatia weledi na elimu yao katika ushiriki wa kujenga uchumi wakati
wa kujadili mada kwenye semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF
juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika
ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti
wa Shirikisho la wenye Viwanda Tanzania CTI Bw. Subhash Patel (wa pili
kulia) akizungumza sheria na vikwazo mbalimbali vinachangia kukwamisha
ukuaji wa sekta binafsi wakati wa kujadili mada kwenye semina ya pamoja
kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi
wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es
Salaam.
Bi.
True Schedvin (kulia) kutoka Ubalozi wa Sweden alisema katika safari ya
Tanzania kuelekea uchumi wa kati ni vyema Tanzania kuangalia mambo
mbalimbali ikiwemo kazi, afya elimu na masoko wakati wa kujadili mada
kwenye semina ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya
Tanzania kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano
wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Mmoja
wa washiriki akiuliza swali kwa wajadili wa mada wakati wa semina ya
pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea
uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini
Dar es Salaam.
Msajili
wa Hazina Dkt. Oswald Mashindano akifuatilia kwa umakini maoni
yaliyokuwa yakiwasilishwa wakati wa semina ya pamoja kati ya Benki ya
Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati
iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
Ofisa
Mtendaji Mkazi wa Benki ya Dunia nchini, Bi Bella Bird akifunga semina
hiyo ya pamoja kati ya Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania
kuelekea uchumi wa kati iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF
jijini Dar es Salaam.
Pichani
juu na chini ni sehemu ya wadau wa maendeleo,sekta binafsi pamoja na
taasisi mbalimbali za serikali waliohudhuria semina ya pamoja kati ya
Benki ya Dunia na ESRF juu ya safari ya Tanzania kuelekea uchumi wa kati
iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ESRF jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment