Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipofungua Kongamano la
Kitaifa la Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto kwenye ukumbi
wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es salaam (DUCE).
Baadhi ya Washiriki wa Kongamano la Kitaifa la Kutokomeza Ukatili dhidi
ya Wanawake na Watoto wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati
alipofungua Kongamano hilo kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha
Dar es salaam (DUCE).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu Tanzania Mstaafu, Bibi Helen
Kijo Bisimba baada ya kufungua Kongamano la Kitaifa la Kutokomeza
Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu
Kishiriki cha Dar es salaam (DUCE). (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewataka wadau
kuunganisha juhudi za pamoja kukabiliana na ukatili dhidi ya makundi ya
wanawake na watoto.
Hayo yamesemwa wakati wa ufunguzi wa Kongamano la kitaifa la kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Majaliwa
amesema serikali imeandaa mwongozo na utaratibu wa usimamizi na
ufuatiliaji unaotoa maelezo kuhusu uundwaji wa kamati mbalimbali za
mfumo wa mawasiliano na uwasilishaji wa taarifa.
“Lengo
kuu la serikali ni kuhakikisha ukatili dhidi ya wanawake na watoto na
makundi kengine unatokomezwa na haki zote zinalindwabna
kuheshimiwa,”amesema Majaliwa.
Pia,
amesema kutakuwa na kamati za kijinsia na ustawi wa wanawake na kwenye
kuunga mkono serikali imefanya jitihada mbalimbali za kufanya kampeni za
kitaifa ili kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto ikiwa ni
pamoja na ndoa za utotoni ikiongozwa na Shirika la Jukwaa la Utu wa
mtoto (CDF).
“Suala
la ukatili dhidi ya wanawake na watoto ni jambo mtambuka na linahitaji
ushitikishwaji wa wadau katika kutokomeza janga hili linaloikabili
nchini yetu.”amesema Majaliwa.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la jukwaa la utu wa mtoto (CDF)Bwn
Koshuma Mtengeti ameiomba serikali kutoa ushirikiano pamoja na kutenga
bajeti ya kutosha katika kuendesha mikakati ya kupinga ukatili wa
kinjisia nchini.
"Mwezi
Mei mwaka 2018, mwalimu wa shule ya msingi hapa jijini Dar es Salaam
alituhumiwa kuwadhalilisha kingono wanafunzi wake wanne wa kike wa
darasa la saba kwa kuwageuza kuwa wake zake na kufanya nao
ngono,”amesema Mtengeti.
Tunakushukuru
sana Mh. Raisi John P. Magufuli kwa salamu zako kutoka kwa Waziri Mkuu,
Mh. Kassim Majaliwa. Tumefarijika kujua kwamba uko nasi bega kwa bega
katika kongamano hili la kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Makamu
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. William Anangisye amesema
Suala la Ukatili dhidi ya Watoto na Wanawake ni nyanja pana, ni tatizo
linalozikabili nchi zote Duniani ingawa viwango vya Ukataili
hutofautiana.
Ripoti
mbalimbali za haki za binadamu zimeweza kuonyesha kuna ongezeko kubwa
la ukatili dhidi ya watoto kwa kipindi cha mwaka 2018 ukilinganishwa na
mwaka 2017 nchini.
Aidha,
kongamano hilo litatoa fursa kwa washiriki kudadavua ukubwa wa sura za
ukatili yanayowasibu wanawake na watoto na litasaidia juhudi za kuweka
mikakati madhubuti ya kuzuia, kukabili na kuanzisha utaratibu wa
kuboresha huduma kwa watoto na wanawake waathirika wa ukatili.
No comments:
Post a Comment