Majukwaa ya Vijana yaliyoko katika kata mbalimbali za Wilaya ya
Arusha yameshiriki katika maonyesho ya Ujasirimali yaliyoandaliwa na
shirika lisilokua la kiserikali la Infoy ambapo vijana hao wameonyesha
shughuli za ufugaji wa samaki na bidhaa za usindikaji.
Mratibu wa Shirika lisilokua la kiserikali la INFOY, Laurent Sabuni
alisema kuwa Maonyesho hayo yanalenga kuhimiza ushiriki wa vijana
katiika uchumi wa viwanda na kuongeza kuwa kutokana na vijana
kuchangamkia fursa ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo suala la
vifungashio linapaswa kutiliwa mkazo ili kuinua ari ya uzalishaji .
Sabuni alisema kuwa Majukwaa ya vijana ni moja ya njia muhimu ya
kuwakusanya vijana na kuwaweka pamoja ili waweze kupata mafunzo ya
ujasiriamali pamoja kuwafikia vijana wengi ambao wana nia
ya kusonga mbele kiuchumi.
“Vijana wakiwa katika vikundi ni rahisi kusaidika tofauti na kuwafikia
kijana mmoja mmoja inakua ngumu hivyo ni vyema vijana wakajiunga
kwenye vikundi” Alieleza Sabuni
Mjasiriamali Goodness Shayo Alisema kuwa maonyesho hayo yatasaidia
kuinua ari ya vijana kujikita katika shughuli za uzalishaji badala ya
kuwa walalamikaji na pia kuondokana na kasumba ya kuchagua kazi.
Alisema kuwa mkoa wa Arusha vijana wamekua wakizalisha bidhaa mbali
mbali licha ya uhaba wa viwanda vya kutengeneza vifungashio vya bidhaa
suala linalowazimu kuagiza kutoka mikoa mingine hivyo kuongeza gharama
za usafirishaji na kuathiri bei ya bidhaa zao katika soko.
Goodness ameiomba serikali na taasisi binafsi kuungana kutatua
changamoto hiyo kwa kuanzisha viwanda vya kutengeza vifungashio
kutokana na mwamko wa vijana wa kuchangamkia fursa za uchumi wa
viwanda kwa kuanzisha viwanda vidogo vidogo vya usindakaji wa nafaka.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha Gabiel Daqqaro akipata Maelezo juu ya
bidhaa zinazozalishwa na vijana kutoka Majukwaa ya Vijana Wilaya ya Arusha
yaliyoandaliwa na shirika lisilokua la kiserikali la INFOY. Picha na
ahmed mahmoud Arusha.
Na Ahmed Mahmoud, Arusha.
No comments:
Post a Comment