Waziri
wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI)
Selemani Jafo amechukizwa kuona baadhi ya viongozi na watendaji
kutotimiza majukumu yao ipasavyo ikiwemo kufanya mambo kienyeji kwa
kupokea miradi ya maendeleo pasipo kufahamu mwenendo mzima wa mkataba
ulivyo pamoja na kutojua gharama za fedha ambazo zinatolewa kwa ajili
ya utekelezaji.
Jafo
ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi katika Kituo cha afya
cha mlandizi kilichopo Wilayani Kibaha mkoani Pwani kwa lengo la
kujieneo mwenendo mzima wa ukarabati wa majengo pamoja na kujionea
ujenzi wa majengo matatu ambayo yamejengwa kwa kiasi cha shilingi
milioni 400 fedha ambazo zimetolewa na serikali kuu.
Pia
Jafo alibainisha kuwa hawezi kuwavumilia watumishi ambao ni wazembe na
wanashindwa kutimiza majukumu yao ipasavyo na kuwataka kuachana mara
moja na vitendo vya kujihusiha na ubadhilifu wa fedha ambazo zinatolewa
na serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya maendeleo.
“Mimi
kama kiongozi wetu sipendi kuona kabisa mnafanya kazi kienyeji bila ya
kuzingatia sheria na taratibu amabzo zimewekwa na nchi, na katika hili
siwezi kulifumbia macho maana maeneo mengine nimepita nimekuta miradi
mingine bado inasua sua nah ii ni baadhi ya watu kutotimiza majukumu yao
ipasavyo ni ninachotaka miradi yote inapokuja lazima wahusika kufahamu
mikatab ailivyo pamoja na fedha ambayo inatolewa sio kupokea tu,”alisema
Jafo.
Aidha
aliseama kwamba serikali ya awamu ya tano kwa sasa imeshatoa fedha
katika vituo vya afya zaidi ya 90 hapa nchini kwa lengo la kuweza
kuongeza majengo mengine pamoja na kufanya ukarabati wa miundombinu ya
wodi mbali mbali ikiwemo nyumba za watumishi kwa lengo la kuweza
kuboresha sekta ya afya kwa wananchi.
Aidha
katika hatua nyingine Jafo ameupongeza uongozi wa halmashauri ya Kibaha
vijijini kwa kutekeleza agizo lake la kukukarabati chumba cha
kuhifadhia maiti katika kituo cha afya mlandizi ambapo hapo awali
kilikuwa hakifanya kazi kabisa kwani kiligeuzwa kuwa eneo la stoo na
kuhifadhia vyuma chakavu.
Kwa
upande wake Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kibaha vijijini
Butamo Nuru alisema kwamba wametekeleza agizo ambalo walipatiwa na
waziri wa Tamisemi la kukarabati miundombinu ya chumba cha kuhifadhia
maiti pamoja na kununua majokofu nane ambayo yamegharimi kiasi cha
shilingi milioni 36.
WAZIRI
Jafo katika ziara yake ya kikazi kwa halmashauri ya Kibaha vijijini
ameweza kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa
majengo matatu ya wodi ya upasuaji,wazazi,na wagonjwa wa nje (OPD)
sambamba na kutembelea miradi mingine miwili ya ujenzi wa hospotali
pamoja na jengo la ofisi za halmashauri hiyo.
Waziri
wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za miko na serikali za mitaa (TAMISEMI)
Seleman Jafo kushoto akimpa maelekezo Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Assumpter
Mshama wa kulia kuhusiana na usimamiza wa fedha zinazotolewa katika
miradi mbalimbali ya maendeleo katikati ni Mbunge wa Jimbo la Kibaha
vijijini Homoud Jumaa mara baada ya kukagua ujenzi wa wodi tatu
zilizojengwa katika kituo cha afya mlandizi pamoja na kujionea
ukarabati wa chumba cha kuhifadhia maiti.

No comments:
Post a Comment