Matokeo chanyA+ online




Tuesday, March 12, 2019

BALOZI WA JAPANI NCHINI TANZANIA ATEMBELEA MAKUMBUSHO YA TAIFA

 Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof. Audax Mabula akimweleza jambo Balozi wa Japani Nchini Tanzania, Shinichi Goto aliye mbele yake alipotembelea Makumbusho ya Taifa (leo asubuhi) Mtaa wa Shabani Robert, jijini Dar es Salaam, wengine ni wasaidizi wa Balozi wa Japani. 
  Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Bi Flower Manase (wa kwanza kushoto) akimweleza Balozi wa Japani Nchini Tanzania, Goto jambo alipotembelea ofisini kwa Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa leo. Kulia kwa Balozi ni Msaidizi wake Bi Brayan Nassoro Salle.
 Balozi wa Japani nchini Tanzania Shinichi Goto (wa kwanza kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Taifa Prof. Audax Mabula na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni, Bi Flower Manase wakifurahia kalanda ya mwaka 2019 iliyotolewa kama zawadi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho na Balozi wa Japani.
  Balozi wa Japani nchini Tanzania Shinichi Goto  akiangalia kompyuta za watoto alipotembelea maktaba ya watoto, iliyopo Makumbusho ya Taifa. Kushoto kwake ni Afisa Elimu wa Makumbusho ya Taifa Anamery Bagenyi.
  Balozi wa Japani nchini Shinichi Goto akisiliza maelezo kuhusu maktaba ya watoto kutoka kwa Afisa Elimu wa Makumbusho ya Taifa, Anamary Bagenyi alipotembelea Makumbusho ya Taifa (leo asubuhi).
 Balozi wa Japani nchini, Shinichi Goto akipata maelezo kutoka kwa Dkt. Amandus Kweka kuhusiania na chimbuko la mwanadamu katika ukumbi wa maonesho wa Chimbuko la Mwanadamu, Makumbusho ya Taifa.
Picha na Maelezo na Joyce Mkinga wa Makumbusho ya Taifa

No comments:

Post a Comment