|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wanachi wa kata ya Isaka waliojitokeza kwa wingi kumlaki wakati akiwasili wilayani Kahama kwenye ziara ya kikazi. | |
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo
tarehe 1, Machi 2019 ameendelea na ziara yake ya kukagua na kuhamasisha
shughuli za maendeleo katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.
Akiwa
Wilayani Kahama Makamu wa Rais alitembelea mradi wa upanuzi wa mtandao
wa maji ya Ziwa Victoria kwennda katika miji ya Kagongwa na Isaka wenye
gharama ya shilingi bilioni 24.72 zikiwa fedha za ndani.
Akizungumza
na wananchi wa kijiji cha Isagehe ambapo pamejengwa matanki mawili ya
maji ambayo yana uwezo wa kubeba lita laki 8 kila moja, Makamu wa Rais
alisema “Serikali ya awamu ya tano inawajali na kuwathamini wananchi
wake na kuwahakikishia wananchi hao maji yatafika kote yalipoahidiwa”
Makamu
wa Rais pia alitembea mgodi wa dhahabu wa Buzwagi na kutaka kufahamu
mgodi huo umejiandaaje kuyaacha mazingira salama mara baada ya kufungwa.
Kwa
upande wake Naibu Waziri Madini Mhe. Stanslaus Nyongo amesema sheria
mpya ya madini itasaidia sana katika kuboresha maisha ya Watanzania
wengi kwani pamoja na kodi itakayolipwa pia wachimbaji wanajukumu la
kuchangia huduma za kijamii kwenye maendeo yanayozunguka mgodi.
Aidha,
Makamu wa Rais aliweka jiwe la msingi la ufunguzi wa madarasa 8 ambao
ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi milioni 121 ikiwa ni miradi ya
TEA na P4R katika shule ya Sekondari Nyashimbi wilayani Kahama.
Mwisho
Makamu wa Rais alihutubia wananchi wa Kahama katika uwanja wa michezo
wa Taifa ambapo alihimiza wananchi hao kushirikiana na Serikali katika
masaula ya maendeleo.
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wanachi wa kata ya Isaka waliojitokeza kwa wingi kumlaki wakati akiwasili wilayani Kahama kwenye ziara ya kikazi. |
|
Matanki mawili ya maji ambayo ni sehemu ya mradi wa upanuzi wa mtandao wa maji ya ziwa Victoria kwenda katika miji ya Kagongwa na Isaka | | |
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akikagua matanki mawili ya maji ambayo ni sehemu ya mradi wa
upanuzi wa mtandao wa maji ya ziwa Victoria kwenda katika miji ya
Kagongwa na Isaka kwa gharama ya shilingi blioni 24.72. |
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na wananchi wa kata ya Isagehe mara baada ya kukagua
matanki mawili ya maji ambayo ni sehemu ya mradi wa upanuzi wa mtandao
wa maji ya ziwa Victoria kwenda katika miji ya Kagongwa na Isaka kwa
gharama ya shilingi blioni 24.72. | | |
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wanachi wa kata ya Isaka waliojitokeza kwa wingi kumlaki wakati akiwasili wilayani Kahama kwenye ziara ya kikazi. | |
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasalimu wanachi wa kata ya Isaka waliojitokeza kwa wingi kumlaki wakati akiwasili wilayani Kahama kwenye ziara ya kikazi. |
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna mazingira yatakavyoachwa mara baada ya mgodi wa dhahabu wa Buzwagi kufungwa kutoka kwa Meneja wa Mazingira na Ufungaji Mgodi Bi. Rebecca Stephen. |
|
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata maelezo ya namna mazingira yatakavyoachwa mara baada ya mgodi wa dhahabu wa Buzwagi kufungwa kutoka kwa Meneja wa Mazingira na Ufungaji Mgodi Bi. Rebecca Stephen. | |
No comments:
Post a Comment